Friday, 31 January 2014

SIKU YA MWISHO YA USAJILI: MAN UNITED NA MAN CITY ZAPIGANA VIKUMBO KUSAINI MABEKI WA PORTO




Manchester United wametuma ofa ya kiasi cha €15 million kwa ajili ya kumsaini beki wa kati wa klabu ya Porto Nicolas Otamendi.

Wakati Porto wakiwa radhi kumuuza beki huyo wa kiargentina kuliko kumuuza beki mwingine wa kati Eliquiam Mangala, bado hawajaamua rasmi kuuza au wasiuze mchezaji huyo.


Otamendi amekuwa kwenye kikosi cha Porto tangu msimu wa 2010/11 wakati timu ilipokuwa chini ya  Andre Villas-Boas' wakati walipotwaa makombe matatu, ukiwa msimu wa kwanza kwa beki huyo.  


Beki huyo mwenye miaka 25 tayari ameshaichezea timu yake ya taifa ya Argentina mechi 16, lakini amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa tangu alipowasili kocha Alejandro Sabella.
  
Hata hivyo, ofa ya United inaweza ikafeli kutokana na wapinzani wao Manchester City kumtaka Mangala, hivyo Porto hawawezi kukubali kuwauza mabeki wao tegemezi wa kati kwa pamoja.

0 comments: