Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana
na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa
jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto
mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini
Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na
jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika
kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto
mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili
waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo
uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya.
Waendesha
Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo.
Msafara
wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya
kuwasili mkoani humo.
Waendesha Bodaboda wakifuatilia hotuba za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea
risala ya waendesha Bodaboda kutoka kwa Msumba Makya Katibu wa Waendesha
Bodaboda.
0 comments:
Post a Comment