>>KUVAA JEZI NAMBA 8!!
>>JUMANNE USIKU KUANZA RASMI NA ROONEY, ROBIN VAN PERSIE!!
MCHEZAJI
MPYA wa Mabingwa Manchester United, Juan Mata, Leo ametambulishwa
rasmi na kupewa Jezi Namba 8 huku mwenyewe akisema bado yapo matumaini
ya kutetea Ubingwa wao.
Man United wapo Nafasi ya 7 kwenye Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal huku Mechi zikiwa zimebaki 16.
Mata, ambae amejiunga na Man United hivi
Juzi akitokea Chelsea kwa Dau la Pauni Milioni 37.1 ambalo ni Rekodi
kwa Man United, huenda akacheza Mechi yake ya kwanza Jumanne Usiku
Uwanjani Old Trafford dhidi ya Cardiff City kwenye Ligi Kuu England
akivaa Jezi yake Namba 8 ambayo kabla ilikuwa ikivaliwa na Anderson
alieenda Fiorentina kwa Mkopo.
Mata, mwenye Miaka 25 na anaechezea Timu
ya Taifa ya Mabingwa wa Dunia Spain, amesema: “Ninachopenda kuhusu
Klabu hii ni ile imani yao ya kutokata tamaa. Ingekuwa Klabu nyingine
iko kwenye hali hii, ingekuwa ngumu kurudi na na kuchukua Nafasi ya
Kwanza, lakini Klabu hii inaweza. Huo ndio msimamo thabiti wa Man
United, Siku zote wanapigania Mataji, Siku zote wanashinda toka hali
ngumu!”
Vile vile, Mata alisema anangojea kwa hamu kucheza na mwenzake Wayne Rooney.
Ameeleza: “Kwangu mimi, yeye ni mmoja wa
Wachezaji Bora katika Historia ya Nchi hii. Huwezi kuamini Uchezaji
wake. Ni Straika anaeweza kufunga, kusaidia kufunga na kurudi kwenye
Kiungo kusaka Mipira. Nitajaribu kushirikiana nae kwa kadri ya uwezo
wangu na kusaka mapengo kwenye Difensi za Wapinzani. Nadhani staili
yangu nzuri ni kufanya hivyo! ”
Mata, ambae alitokea Valencia ya Spain
na kujiunga na Chelsea ambayo aliifungia Mabao 32 katika Mechi zaidi ya
130, ameichezea Timu ya Taifa ya Mabingwa wa Dunia Spain Mechi 32.
Akiongelea ujio wa Mata, Meneja wa Man
United David Moyes amesema ameshangazwa kuweza kumsaini Mchezaji Bora
kama Juan Mata kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari.
Moyes amesema: “Nimefurahishwa.
Tulidokezwa Mwezi mmoja au miwili nyuma lakini sikutegemea kama
tutafanikiwa. Tulipopata nafasi kumchukua tuliingia moja kwa moja.
Watakuja Wachezaji kama yeye baadae.”
ROBIN VAN PERSIE NA WAYNE ROONEY WARUDI!
Wayne Rooney na Robin van Persie
wanaweza kurudi kuichezea Manchester United Jumanne Usiku Uwanjani Old
Trafford dhidi ya Cardiff City kwenye Ligi Kuu England.
Rooney amekuwa nje ya Uwanja tangu
Januari Mosi Man United walipofungwa na Tottenham alipoumia Nyonga na
Van Persie yuko nje tangu Desemba 10 alipoumia Paja kwenye Mechi ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Lakini Mastaa hao wawili wamepona na
huenda wakapangwa pamoja na Mchezaji mpya Juan Mata dhidi ya Cardiff
City ambayo ipo chini ya Meneja Ole Gunnar Solskjaer, Nguli wa Man
United, ambae ni Meneja mpya hapo Cardiff City.
0 comments:
Post a Comment