Mlipua mabomu wa kujitoa muhanga ameuwa watu wapatao 5 katika makao makuu ya Polisi katika mji mkuu wa Misri, Cairo, mabomu matatu ya kwanza kupiga mji huo mapema Ijumaa. (JM)
Maafisa wa usalama wanasema
mshambuliaji huyo alijilipua kwenye eneo la kuegesha magari la kati kati
ya mji katika mashambulizi makubwa nchini humo katika miezi kadhaa.
Saa chache baadaye maafisa wanasema
mlipuko mwingine karibu na kituo cha treni upande wa pili wa mto Nile
uliua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Wizara ya mambo ya ndani inasema
shambulizi la tatu lilitokea huko Giza karibu na kituo cha Polisi kwenye
bara bara kuu iendayo kwenye mapyramid lakini hakukuwa na majeruhi.
CHANZO SAUTI YA AMERIKA
0 comments:
Post a Comment