Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ulikuwa ni
‘uamuzi mgumu’ kwake kumwachilia mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya
taifa ya Hispania Juan Mata kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya
England Manchester United.
Mata aliye na umri wa miaka, 25, ameweka rekodi ya uhamisho katika
klabu ya Man United kwa baada ya kuuzwa na Chelsea kwa kitita cha pauni
milioni 37.1.
Akizungumza na BBC Mourinho amesema:
” Haya ni maamuzi ambaye mkufunzi anapaswa kufanya, lakini kwangu
ilikuwa vigumu. Ningependa kuendelea kumuona katika kikosi changu bila
shaka,”
“Lakini kuwa katika hali hii kwa mchezaji ni vigumu. Anastahili
kuachiwa milango wazi katika Chelsea. Napenda kuwaona watu wakiwa na
raha. Nasikitika sikuweza kumfurahisha katika kikosi hiki – nasikitika
sana kwa hilo, lakini najenga kikosi changu nikizingatia mchezaji Oscar
ambaye anacheza katika nafasi ya 10,” anasema mzee Mourinho.
0 comments:
Post a Comment