>>NI KESI YA NGONO NA ‘CHANGU’ CHINI YA UMRI HALALI!
KESI
ya Mastaa wa France, Franck Ribery na Karim Benzema, waliokuwa
wanashitakiwa kwa kutembea na Changudoa alie chini ya Umri halali,
imefutwa hii leo huko Paris, France.
Ribery, Miaka 30, Winga wa Bayern
Munich, na Straika wa Real Madrid Benzema, Miaka 26, wote walikanusha
Mashitaka kuwa walilipia ngono kwa Mwanadada Zahia Dehar wakati akiwa
chini ya Miaka 18.
Wachezaji hao wawili walishitakiwa kwa
kutembea na Dehar akiwa na Miaka 16 kwenye Kesi ya Benzema na Miaka 17
kwenye Shitaka la Ribery.
Huko France, Kisheria, ngono na Msichana
alie zaidi ya Miaka 15 ni halali lakini kulipia ngono kwa Msichana alie
chini ya Miaka 18 ni Kosa la Jinai.
Kulipia ngono kwa Msichana alie zaidi ya Miaka 18 ni ruksa.
Kesi iliendelea licha ya Mahakama ya Juu
huko France kutoa msimamo kuwa ni wale wanaojua kuwa Msichana yuko
chini ya Umrii halali ndio washitakiwe kwa kuvunja Sheria.
Wakati Ribery alikiri kutembea na Dehar
lakini hakujua kuwa yuko chini ya Miaka 18, Benzema yeye alikanusha moja
kwa moja kuwahi kukutana na Dehar.
Dehar, ambae sasa ana Miaka 21, alitoa
Ushahidi kuwa alifanya ngono na Wachezaji hao na kulipwa Fedha baada ya
kuwadanganya Umri wake.
0 comments:
Post a Comment