Thursday, 30 January 2014

UHAMISHO SIKU YA MWISHO: TONI KROOS NJIANI OLD TRAFFORD??

>>APANDWA JAZBA ALIPOBADILISHWA MECHI NA STUTTGART!!

>>PEP ANENA: “LEO YUKO HAPA, KESHO AMETIMKA!!”
TONI_KROOS2HUKU Dirisha la Uhamisho likifikia Siku yake ya mwisho Ijumaa Januari 31, huko Germany kunatikisika kwa habari kuwa huenda Kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos, huenda akatua Manchester United kufuatia kauli ya Meneja wa Mabingwa hao wa Germany, Pep Guardiola.
Akiwa bado amebakisha Miezi 18 kwenye Mkataba wake wa sasa na Bayern, Toni Kroos, Miaka 24, amekataa kuongeza Mkataba mpya akidai nyongeza kubwa ya Mshahara ambayo Klabu hiyo inagoma kumpa ili kukwepa kuibua malamiko ya Wachezaji wengine.
Jana Mchezaji huyo alionyesha hasira za wazi Uwanjani pale alipovua Glovu zake na kuzitupa kwenye Benchi la Bayern wakati alipobadilishwa kwenye Mechi ya Bundesliga na Stuttgart huku Bayern iko nyuma Bao 1-0 lakini iliibuka Washinda Bao 2-1 baada Thiago Alcantara kufunga Bao tamu la ushindi katika Dakika ya 93.
Wiki moja iliyopita, Meneja wa Manchester United, David Moyes, alikwenda kumtazama Toni Kroos akicheza wakati Bayern Munich inaifunga Borussia Monchengladbach Bao 2-0 huku Moyes akinaswa akiongea na Wakala wa Kroos, Sascha Breese.
Inaaminika anaweza kuihama hivi sasa Bayern Munich kwa Dau la kati ya Pauni Milioni 20 hadi 25 huku kukiwa na tetesi akiwa Old Trafford atalipwa Pauni 150,000 kwa Wiki ambazo Bayern inagoma kumlipa.
Na Meneja wa Bayern, Pep Guardiola, amekaririwa akisema: “Ni Mchezaji muhimu lakini kwenye Soka vitu huenda haraka. Leo yuko hapa, kesho ameondoka!”
Toni Kroos, ambae ameichezea Germany mara 41, Msimu huu ameanza Mechi 15 za Bundesliga kwa Bayern lakini anakabiliwa na upinzani mkali wa namba kwenye Kiungo kutoka kwa Thiago, Javi Martinez, Bastian Schweinsteiger na Philipp Lahm.

0 comments: