Wizara ya utumishi wa umma imetuma
waraka unaotoa mwongozo wa mavazi kwa watumishi wote wa ofisi za umma na
wananchi wote wanaohitaji huduma ktk ofs hizo.
Waraka huo namba 3 wa mwongozo wa mavazi wa mwaka 2007 unawatka
wafanyakazi wote wa ofisi za umma na wananchi wote kutokuvaa mavazi
yafuatayo:-
-Jeans
-Nguo zenye maandishi yoyote
-Nguo zinazobana mwili wako
-Nguo zilizo juu ya magoti (sketi/gauni)
-Kaptula
-Pedo
-Jezi za timu za mpira
-Nguo za chama chochote cha siasa
-Suruali ambazo hazijapindwa
-Blauz zinazoacha kifua/mgongo wazi
-Kuvaa mlegezo
Waraka huo ulikuwepo ila uekelezaji haukufanyika,hivyo kwanzia mwaka huu utaanza kutumika nchi nzima.
Wananchi usiende ofisi za umma ukiwa umevaa mavazi tajwa hapo juu,utaishia kufukuzwa bila kuhudumiwa(Na JF)
0 comments:
Post a Comment