Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA ) Absalom Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri amesema maamuzi ya mahakama hiyo yamerejesha matumaini mapya kwa tasnia ya habari kwa wanahabari na vyombo vya habari kwamba pamoja na sheria kandamizi wanayo fursa ya kushinda baadhi ya hila, baadhi ya mipango ya kudhulumu vyombo vya habari nchini Tanzania.
Akielezea maamuzi ya mahakama hiyo amesema kwamba mahakama iliamua kuwa serikali ilifungua kesi hiyo katika misingi ya hisia kwani yalioandikwa ni masuala ya kawaida hakukuwa na nia ya uovu, waandishi walitumia uhuru wao wa kujieleza na hakukuwa na matukio yeyote ya wazi kwamba baada ya ile makala kumekuwa na vitendo au matukio yaliotokana na uandishi wa makala hiyo.
Amesema maamuzi hayo yatalazimisha mabadiliko kwani ni sawa na kujifunza kwa viboko kwani kuna dhamira mbaya na chuki za wazi dhidi ya vyombo vya habari, ni fundisho kwamba lazima walio madarakani, waandishi na wananchi wa kawaida wanapaswa kujifunza kwamba hakuna aliye juu ya sheria.
Amesema wana imani kupitia mchakato wa katiba mpya kuwa wataweza kupata fursa ya kuingiza masuala mengi yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari katiba katiba mpya ijayo nchini humo.
Akielezea zaidi kuhusu chuki dhidi yao amesema upande mmoja ni kwasababu ya waandishi wenyewe na kwa upande mwingine viongozi walioko madarakani hawapendi kukosolewa kutokana na tabia zao akitolea mfano matumizi mabaya ya madaraka ya Polisi.
Chanzo, voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment