Friday, 31 January 2014

SAMATTA MCHEZAJI BORA WA MWAKA TP MAZEMBE



Samata-Bwana58021_6e83d.jpg

MBWANA Ally Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2013 wa klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mshambuliaji huyo wa Tanzania, maarufu kama Sama Goal amewashinda Solomon Asante na Robert Kidiaba alioingia fainali.
Samatta alipata kura 248, Asante Solomon kura 219, Robert Kidiaba kura 200, Nathan Sinkala kura 97 na Rainford Kalaba kura 67.
Mafanikio hayo yametokana na Samatta kuwa tegemeo la mabao la Mazembe kuanzia Ligi Kuu ya DRC, Ligi ya Mabingwa na baadaye Kombe la Shirikisho, ambako timu hiyo ilifika fainali. Mazembe inaye Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu.

0 comments: