Thursday, 30 January 2014

NANI ANA TENDA YA KUSAFISHA MITARO NA BARABARA ZA KIRUMBA JIJINI MWANZA??


Nazungumzia kampuni yenye dhamana ya kusafisha mitaro ya maeneo ya Kirumba jijini Mwanza, muhusika yapata wiki ya pili sasa tunaenda ya tatu ametoa mchanga, takataka na tope zilizokuwa kwenye mifereji na kuzirundika kandokando ya barabara bila kuzizoa.

Lundo hili la udongo toka kwenye mifareji ya maji taka halileti taswira nzuri kwa barabara hii ya pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba kuelekea barabara kuu ya Makongoro Air port kupandisha kuelekea Kanisa la Roman Kirumba, Yaani ni uchafu hata barabara yenyewe iliyojengwa kwa kiwango cha lami inakosa maana. 
Ingawa ni barabara kiwango cha lami, magari yakipita ni vumbi kwa kwenda mbele .
Taswira hailipi kabisa....
Wana kusanya lakini hawazoi tatizo nini?
Taratibu wapitao wanazikanyaga taka hizo, je kwa style hii zitasalimika kurudi kwenye mitaro mvua ikinyesha? Work done zero. Au twataka tenda nyingine kuendelea kula fedha za Manispaa?
'Tenda za kupeana hazina kukoromeana' Funika kombe mwanaharamu apite maisha yaendelee.(picha na mpigapicha wa    kanda ya  ziwa Bw  wiliam Bundala)

0 comments: