YA MUFINDI NA IRINGA KIKAONI
Wenyeviti hao wameonyesha kutofautiana wakati wa kikao cha kamatin ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ambapo diwani Mhapa alionyesha kupinga kwa nguvu zote matumizi ya mbolea hiyo na kutaka wananchi kurejeshewa pesa zao asilimia 41 walkiochangia kwa ajili ya pembejeo huku mwenyekiti mwenzake Tweve akipinga.
Awali mkuu wa mkoa alisifu matumizi ya mbolea hiyo kuwa ni mbolea nzuri inayoongeza kasi ya uzalishaji wa mazao na hata kumtaka Mhapa kusimama kutoa ushuhuda katika kikao hicho jinsi ambavyo anavyoweza kuvuna gunia 30 kwa hekari moja jambo ambalo alidai ni mafanikio ya minjingu mazao na hivyo kumsimamisha kuelezea wajumbe mafanikio hayo .
" Kwanza utanisamehe mheshimiwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa sikukusimamisha mapema kuelezea jinsi unavyopata magunia 30 kwa hekari moja hebu sasa simama uwaelezee wajumbe ili kuwapa matumaini wananchi " alisema mkuu huo wa mkoa.
Hata hivyo mhenyekiti huyo Mhapa hakuweza kueleza mafaniko hayo na badala yake alianza kwa kusema anasikitika sana kuona serikali ikilazimisha kutumia mbolea hiyo huku wananchi wakiendelea kuikataa .
"Kwa masikitiko makubwa ndugu mwenyekiti ninaomba serikali kuwarudishia wananchi fedha zao walizochangia asilimia 41 kwani mbolea hii ni bomu na wananchi wanahisi kuwa serikali imewafanyia utapeli wa fedha zao....mimi naomba serikali irudishe fedha za wananchi kwani tabu kubwa tunaipata sisi viongozi wa chini ambapo wananchi hawatuelewi na kutuona sisi pamoja na chama changu CCM ni matapeli...ninaomba kama hakuna faida ya cha juu asilimia 10 ambayo viongozi wanaopigia debe wanapata basi wananchi wapewe fedha yao"
Mhapa alitaka wakulima kujichagulia mbolea wanayoitaka na serikali kuweka ruzuku katika mbolea zote badala ya kulazimisha kutumia mbolea hiyo ya Minjingu mazao ambao hakifai hata kidogo.
Huku mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Bw Tweve akiipongeza serikali kwa mbolea hiyo kuwa ni nzuri na katika Halmashauri yake ya Mufindi wanakitumia na imesaidia sana kuongeza uzalishaji wa mazao.
" Kweli naipongeza serikali kwa mbolea hii kwetu Mufindi mbolea hii inasaidia sana kuongeza uzalishaji wa mazao"
Wakati huo huo Mhapa alisema kuwa hadi sasa katika Halmashauri hiyo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa alijitolea kujenga mabweni 8 katika jimbo la Kalenga ila hadi sasa ni bweni moja pekee ambalo limejengwa na wahusika kwa sasa wamesimama na mbaya zaidi wahusika wa ujenzi huo hawajui lugha ya kiswahili wala Kiingereza sasa imekuwa ni shida sana kujua kama wataendelea kujenga ama vipi.
Hata hivyo alisema anampongeza sana mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge ambae amejaribu kuwasaidia kwa kukutana na mkalimani wao na boss wao ambapo jitihada bado zinaendelea chini ya Lukuvi.
0 comments:
Post a Comment