Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara mkoa wa Iringa katika kikao cha bodi ya barabara leo mjini Iringa |
Wajumbe wa bodi ya barabara mkoa wa Iringa wakimkumbuka aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa |
Wajumbe wakiwa katika kikao hicho leo |
WAKATI kasi ya vitendo vya rushwa katika maeneo ya mizani nchini ikiendelea kuchukua kasi kubwa wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADS ) wameanza kupambana na watumishi wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa katika maeneo ya mizani kwa kufunga kamera maalum aina ya CCTV katika mzani wa Wenda kwenye barabara kuu ya Iringa - Mbeya.
Akizungumza mkakati huo leo katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo meje wa Tanroads mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa alisema kuwa hatua ya ofisi yake kufunga kamera hizo maalum ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa katika eneo hilo la mizani pia kuepusha uharibifu wa barabara unaotokana na baadhi ya watendaji wa ofisi yake wasio waaminifu ambao wamekuwa wakipokea rushwa na kuacha magari yenye mizigo mizito kupita .
Hivyo alisema kupitia kamera hizo ambazo zimefungwa kila kona za eneo hilo la mizani TANROADS itaweza kuwakamata wafanyakazi wanaoomba rushwa katika eneo hilo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Meneja huyo alisema kuwa moja kati ya malalamiko makubwa kwa ofisi yake katika eneo hilo la mizani ni kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa kutoka kwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu kujinufaisha kwa kuomba na kupokea rushwa .
" Kumekuwepo na malalamiko sana kutoka kwa wadau wa usafiri kuwa eneo hilo linajihusisha kwa rushwa hivyo sasa tayari tumeanza kufunga kamera maalum zitakazosaidia kuwabana watumishi wanaoomba na kupokea rushwa na tayari mafundi wanaendelea na kazi hiyo ya kumalizia kufunga kamera hizo"
Pia meneja huyo wa TANROADS alisema kuwa mkoa wa Iringa umeendelea kutekeleza ahadi za Rais Jakaya Kikwete kwenye ilani ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kutekeleza ujenzi wa barabara za mji wa Mafinga kilometa 2 kwa kiwango cha lami ,ujenzi wa barabara ya Sokoni na Msikitini yenye urefu wa Km 1.6 huku TAMISEMI ikiahidi kutenga fedha kukamilisha Km 0.4 zilizobaki.
Aidha ujenzi wa barabara ya Ipogolo- Kilolo yenye urefu wa Km 35 ambayo kazi ya usanifu wa barabara yote ilikamilika mwaka wa fedha 2008/09 na kuwa kiasi cha km 5.8 zimejengwa na Km 1.5 zitajengwa mwaka wa fefha 2013/2014 kwa kazi hiyo kuendelea .
Kuhusu ujenzi wa Km 12.5 za barabara za kalenga ambazo zipo katika ahadi ya Rais Kikwete amesema ujenzi huo umekamilika wakati akisi cha Tsh milioni 635 zilitengwa mwaka wa fedha 2013/14 kuendelea ujenzi wa km 1.0 na kuwa ahadi zinatekelezeka sambamba na ahadi ya ujenzi wa barabara ya Iringa hadi hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye urefu wa Km 104 kwa kiwango cha lami.
Lyakurwa alisema kuwa pia zoezi la kuimarisha miundo mbinu ya barabara za jimbo la Isimani unaendelea kwa barabara za Izazi- Pawaga- Mowa yenye urefu wa Km 83 imepangwa kufanyiwa upembezi yakinifu na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami ambapo fedha iliyotengwa mwaka 2013 /14 ni Tsh milioni 112
Wakati ahadi ya Rais Kikwete ya mwaka 2010 ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara jimbo la Ismani mhandisi mwelekezi M/s Engineering Research Associate toka jijini Dar es Salaam ameshapatikana kwa gharama ya Tsh milioni 172 ambae atafanya kazi kwqa miezi sita na kazi hiyo inatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kukamilika kwa taratibu za mkakaba.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma mbali yakupongeza hatua ya TANROADS kuweka kamera hizo za kupambana na watumishi wala rushwa bado alisema kuwa kuna haja ya ofisi hiyo ya TANROADS kuwabana wenye malori makubwa ambayo yameendelea kupita katika mji wa Iringa katika barabara ya Iringa- Dodoma barabara ambayo hata hivyo bado kukamilika .
Kwani alisema kuwa mbali ya serikali kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo ya Iringa- Dodoma ambayo bado kukabidhiwa ila bado kuna idadi kubwa ya malori yenye mizigo mizito kuendelea kupita katika barabara hiyo hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa uhai wa barabara hiyo .
Hivyo alitaka uongozi wa TANROADS mkoa wa Iringa kuweka zuio kwa wenye malori kuendelea kuitumia barabara hiyo ya Iringa -Dodoma kwa sasa kabla ya kukabidhiwa rasimi .
Kuhusu malalamiko ya madereva katika maeneo ya mizani kwa mizani kutoa majibu tofauti kwa uzito wa magari ,mkuu huyo wa mkoa alitaka kujua sababu ambazo zinapelekea mizani hiyo kuwa na majibu tofauti ambapo gari lililopimwa mzani A na kjukutwa na uzito stahiki bado akipima eneo jingine mzigo huo huo unaonekana umezidi uzito.
katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuachana na siasa zaidi na badala yake kusaidia kunusuru uhai wa barabara katika eneo la Ndiuka ambalo linaongoza kwa uharibifu wa barabara kwa watu kuoshea magari barabarani .
Alitaka siasa iende sambamba na maendeleo na katika masuala ya maendeleo ya Taifa ni vema madiwani hao kuachana na siasa na kusimamia maendeleo kwa faida ya wananchi wanaowatumikia .
Pia mkuu huyo wa mkoa alipiga marufuku madereva wa magari wanatumia barabara za mkoa wa Iringa kuachana mara moja na tabia ya kutumia matawi ya miti kama alama ya pembe tatu pindi magari yao yanapoharibika njiani.
Alisema mbali ya suala hilo kuongeza uchafuzi wa mazingira ila bado matumizi mabaya ya alama za barabarani yanachangia uchafuzi wa mito ambayo inatumika kwa matumizi ya binadamu pia.
Wakati huo huo mwakilishi wa mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Victor Mushi ambae ni diwani wa kata ya Mtwivila na mwenyekiti wa chama cha makandarasi mkoa wa Iringa alimtaka meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa kufika katika eneo la bwawa la Kihesa Kilolo na kuangalia kama bwawa hilo lina faida ama halina faida katika eneo hilo na kama lina faida basi kuliwekea mikakati ya kuliboresha na kama halina faida kukaushwa kabisa eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa vifo vya wananchi wanaotumbukia katika bwawa hilo.
0 comments:
Post a Comment