Jana Kiungo wa ulinzi kutoka timu ya Yanga Athuman Idd Athuman maarufu kama
‘Chuji amerejeshwa kundini kuungana na wachezaji wenzake baada ya kuwa
amesimamishwa na uongozi kutona na kitendo cha utovu wa nidhamu
aliouonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
Chuji alisimamishwa na uongozi na Yanga baada ya kuonyesha utovu wa
nidhamu kwa kuamua kuondoka vyumbani kuelekea nyumbani kabla ya mchezo
kumalizika kitu ambacho alikiri ni makosa mbele ya uongozi.
Uongozi wa Yanga ulifikia hatua ya kumpa barua ya kumsimamisha Chuji
ambaye alikiri kufanya kosa hilo na kisha kuandika barua ya kuomba
msamaha na kuahidi kutorudia tena kitendo hicho au kufanya kitendo
kingine chochote cha utovu wa nidhamu.
Baada ya kuandika barua kwa uongozi kuomba msamaha, Chuji alipewa
onyo kali na uongozi na kupewa kipindi cha matazamio ambapo kwa kipindi
cha mwezi mmoja ameonekana kubadilika na kurejea katika nidhamu ya hali
ya juu ndani na nje ya uwanja.
Chuji ataungana na kikosi cha Young Africans kesho tayari kwa
mikikimikiki ya Ligi Kuu pamoja na mashindinao ya Klabu Bingwa Afrika
ambayo yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo kwa Yanga kuanza na
timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro.
0 comments:
Post a Comment