Madakatri
wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa
kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.
Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.
Pia
TFF itatoa kwa madaktari hao fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji
ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu
imeelekeza.
Hakuna
mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za
Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo
utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji.
VPL KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Januari 29 mwaka huu)
kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini.
Kiingilio
katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na
Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani
Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.
Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar
na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.
0 comments:
Post a Comment