Dk Slaa akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya wanne kushoto kwake waliojiunga katika chama hicho jana( |
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa
amesema hawaogopi kuita Baraza Kuu la chama hicho ili kusikiliza rufaa
ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kama inavyodaiwa na baadhi ya
watu.
Alisema
chama hicho kitaitisha kikao hicho hivi karibuni ili kusikiliza utetezi
wa Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
Akihutubia
mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake katika uwanja
wa Mbwetogwa juzi , Dk Slaa alisema Zitto alivuliwa nafasi zake za
uongozi ndani ya chama hicho baada ya kubainika amekiuka maadili ya
chama.
“Hata
nikiwa mimi aua Mwenyekiti wangu Freman Mbowe au kiongozi mwingine
yoyote yule au mwanachama, akikiuka maadili ya chama ni lazima
achukuliwe hatua za kinidhamu,” alisema.
Alisema
hivisasa Zitto aruhusiwi kufanya shughuli za kichama kupitia jukwaa la
Chadema kwa kuwa si kiongozi tena wa Chadema, rufaa yake haijasikilizwa
na kafungua kesi mahakamani.
“Wanachama, wapenzi na wadau wote wa Chadema msimpe ushirikiano wowote Zitto mpaka sula lake litakapohitimishwa,” alisema.
Alisema
oparesheni ya M4C Pamoja Daima haifanywi na chama hicho kwa ajili ya
kusmshughulikia Kabwe, inafanywa ikiwa ni maandalizi yao ya kuelekea
uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Akinukuliwa na gazeti la jamboleo la jana, Kabwe amesema hakuna wa kumzuia kufanya mikutano nchini.
Kwa
kupitia taarifa ya gazeti hilo alinukuliwa akisema “kama kuna mtu
anadhani sitaweza kufanya mkutano wa aina yoyote katika maeneo
mbalimbali nchini anajidanganya, nitazunguka kuzungumza na wananchi kwa
maslahi ya taifa hili na ni haki yangu kikatiba.”
Alisema atafanya mikutano hiyo kama mbunge kwa kuwa ni wajibu wake kikatiba kuzungumza na wananchi kuhsusu mambo mbalimbali.
Wengine
waliohutubia mkutano huo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kawe Dar es Salaam, Halima Mdee.
Viongozi
hao walitumia fursa waliyopewa kujibu hoja mbalimbali zinazotolewa na
viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa zikimponda mbunge wa
jimbo la Iringa Mjini anayedaiwa kashindwa kutekeleza ahadi zake
alizotoa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Katika mkutano huo, Dk Slaa pia aliwapokea na kuwapa kadi za Chadema, wanachama wanne kutoka CCM, TLP na NCCR- Mageuzi.
0 comments:
Post a Comment