Thursday, 30 January 2014

KATA ZA WILAYA YA KARATU ZATAKIWA KUANZISHA MIRADI ILI KUONGEZA UCHUMI KUANZIA NGAZI YA KAYA

images 
Na GLADNESS MUSHI , KARATU
………………………………………………………………….
CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimeagiza uongozi

wa kata zote ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha kuwa inabuni miradi ya

maendeleo ambayo itawasaidia wananchi kuweza kujiongezea kipato lakini

pia kuweza kuondokana na umaskini katika kata zao
Hayo yameelezwa na Katibu wa chama hicho kwa wilaya ya Karatu, Bi Elly
Minja wakati akiongea kwenye harambee ya ujenzi wa jengo la Kitega

uchumi ambalo lipo wilayani humo ambapo pia harambee hiyo ilienda

sanjari na mazoezi mengine mengi ya kuazimisha kuzaliwa kwa CCM hapa

nchini
Bi Elly alisema kuwa kuna haja sasa ya kila kata kuhakikisha kuwa
inakuwa na miradi tena endelevu ambayo itaweza kuwasaidia wananchi

kuondokana na dhana ya umaskini ambayo ikwa sasa ni tishio kubwa sana

kwenye baadhi ya familia.
Alifafanua kuwa miradi hiyo ambayo inatakiwa kubuniwa na wananchi kwa
kushirikiana na viongozi wa kata mbali na kuweza kuwaokoa wananchi

kwenye suala zima la umaskini lakini pia itachangia sana kuongezeka

kwa uchumi wa wilaya hiyo ya Karatu.
Mbali na uanzishwaji wa miradi kwenye kata zote za Karatu pia alisema
kuwa kwa upande wa Jengo la Kitega uchumi lililopo Karatu nalo

litaweza kuwasiaida sana wananchi katika kuboresha uchumi wao lakini

pia litakuwa na faida sana
“uwepo wa jengo hilo la kitega uchumi hapa Karatu ni ishara kuwa sasa
uchumi wa mji wa karatu utaongezeka sana na utaweza kuwasaidia sana

wananchi wa eneo hili hivyo basi wananchi wanatakiwa watumie fursa

ambazo zipo zaidi na sisi tutaendelea kuwa wabunifu zaidi kwa ajili ya

kuweza kuwasaidia wananchi wetu hususani kwenye suala zima la Uchumi

wao wa kila siku”aliongeza Bi Elly
Aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo ya Karatu kuhakikisha kuwa
wanaendelea kutumia vema fursa za  maendeleo ambazo zinatolewa na

chama hicho lakini pia wasikubali kupotoshwa juu ya jitiada ambazo

zinafanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya jamii nzima
Hataivyo Harambee hiyo ilienda sanjari na mazoezi mbalimbali kama vile
ya upandaji miti,ufanyaji wa usafi wa mazingira pamoja na matembezi

ikiwa ni maazimisho ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi hapa nchini.

0 comments: