Katibu
wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo
mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya ikiwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya
CCM ambayo kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mbeya.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimuonyesha Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sehemu ya kuweka jukwaa la waandishi wa
habari kwenye uwanja wa Sokoine ambapo sherehe za miaka 37 ya CCM
zitasheherekewa kitaifa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa
maandalizi ya awali katika uwanja wa Sokoine ambao unategemewa kufanyika
kwa sherehe za mika 37 ya CCM tarehe 2 mwezi wa
februari mwaka huu,mgeni wa heshima anategemewa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kurekebisha uwanja wa
Sokoine ili uweze kutumika vizuri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM .
Picha na Adam H. Mzee
0 comments:
Post a Comment