Viongozi wa Afrika wameanza
mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao
kuu itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan
Kusini.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa tume ya
Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni
wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili
kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.
Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa tangu waasi kuipindua serikali.
Katika taifa jirani ya Sudan Kusini, makundi
hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano
makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati
ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.
Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa
chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu
nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo
hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara.
Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota
katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati
na Sudan Kusini.
Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.
Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini
Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi
katika kipindi cha miaka minne.
0 comments:
Post a Comment