HOME »
» MKULIMA MKAZI WA NYAMHANGA IRINGA MJINI AKUTWA AMEJINYONGA
|
MKAZI
wa Nyamhanga kata ya Kitwiru mjini Iringa Bw Daud Malongo (84)
aliyekuwa akijishughulisha na kilimo amekutwa amefariki dunia baada ya
kujinyonga kwa kutumia kipande cha pazia.
Mwandishi wa mtandao huu wa Iringa Diana Bisangao anaripoti
kuwa Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 27 januari majira ya saa
9:30 jioni.
Kamanda
Mungi ameuambia mtandao huu umebaini kuwa marehemu alikutwa
ndani ya stoo ya nyumbani kwake akiwa tayari ameshafariki huku chanzo
cha tukio hilo la kusikitisha bado hakijafahamika.
katika
tukio lingine JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia Isaya Kimanga
(30) raia wa DRC Congo kwa kosa la kuingia Nchini bila kibali.
Kamanda
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 26 januari katika
Kijiji cha Mtua tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo ambapo askari polisi
walikuwa doria.
|
0 comments:
Post a Comment