Thursday, 30 January 2014

CHAN 2014 FAINALI: GHANA NA LIBYA ZITACHEZWA FEBRUARI MOSI SIKU YA JUMAMOSI


CHAN2014_LOGOMTU 10 Ghana wametinga Fainali ya CHAN2014 baada ya kuibwaga Nigeria kwa Mikwaju ya Penati 4-1 kufuatia Sare ya 0-0 baada Dakika 120 kwenye Mechi iliyochezwa Jana huko Free State Stadium, Nchini Afrika Kusini. .
Jumamosi, Ghana, ambao hii ni Fainali yao ya pili  baada kufungwa na Congo DR Mwaka 2009, watacheza Fainali na Libya ambayo nayo hiyo Jana iliitoa Zimbabwe kwa Penati 5-4.
Ghana walifunga Penati zao kupitia by Michael Akuffo, Theohilus Anobaah, Samuel Ainooson na Abraham Attobrah na Nigeria kufunga yao moja kupitia Christantus Ejike na Kipa wa Ghana, Stephen Adams, kuokoa Penati ya  Solomon Kwambe wakati Ugonna Uzochukwu alipiga juu.
Ghana walipata pigo katika Dakika ya 64 wakati Beki wao Kwabena Abdesuei alipotolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada Kadi za Njano mbili.
VIKOSI:
GHANA: S.Adams,K.Adusei, S.Ainooson, M.Akuffo,J.Opoku (S.Mohammed), S.Bansey (A.Mohammed), A.Attobrah, T.Anobaah, J.Tijani, N.Sulley, Y.Mohammed (S.Afful)
NIGERIA: C.Agbim, K.Solomon, U.Uzochukwu, K.Odunlami,A.Egwuekwe, C.Ejike, R.Ali (J.Obaje),A.Ibrahim (D.Pyagbara), B.Eseme, A.Shehu, I.Ede (B.Imenger)
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Cape Town Stadium]
Morocco 3 Nigeria 4 [3-3 baada Dakika 90]
Mali 1 Zimbabwe 2
Jumapili Januari 26
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
Ghana 1 Congo DR 0
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
Zimbabwe 0 Libya 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 5-4]
2130 Ghana 0 Nigeria 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Ghana yashinda Penati 4-1]
Jumamosi Februari 1
[SAA za Bongo]
Mshindi wa Tatu
1800 Zimbabwe v Nigeria [Cape Town Stadium]
Fainali [Cape Town Stadium]
2100 Libya v Ghana

0 comments: