Kama kuna mikakati iliyobuniwa kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu nchini, ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari za kata.
Pamoja na udhaifu wa shule hizo kama unavyojulikana kwa watu wengi, angalau sasa watoto wengi wa kike wanapata fursa ya kukaa shuleni kwa miaka minne badala ya kuozwa na kuwa mama katika umri mdogo na kuwa mwisho wa elimu yao.

Hata hivyo, mkakati huu pekee haujawa
mwarobaini wa changamoto zinazowakabili watoto wa kike katika safari yao
ya kuelekea kupata elimu. Bado kuna tatizo kubwa la umasikini
uliokithiri na unaokuzwa zaidi na janga la Ukimwi katika jamii ya
Kitanzania kiasi kwamba baadhi ya wasichana wanaoingia shule za
sekondari hawaendelei muda mrefu.
Hawa wanalazimika kuacha shule ama mwanzoni au katikati kwa kukosa ada ama mahitaji mengine ya shule. Watoto wengi ni yatima na katika maeneo yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa na tatizo la Ukimwi hata ndugu na jamaa wamelemewa na mzigo. CHANZO MWANANCHI
Tatizo hili nimeliona Mkoa wa Iringa na sehemu nyingine nchini. Kama utafiti ungefanyika kujua ukubwa wa tatizo hili ingekuwa ni jambo jema. Kwa hiyo, Serikali haina budi kubuni mikakati ya kuwapa fursa wasichana wa kutoka familia maskini na mayatima kumaliza elimu ya sekondari na vyuo vikuu.
Huko nyuma kumekuwepo mifuko ya misaada kama ule wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA) na mingine, lakini kuna baadhi ya viongozi serikalini walipenyeza watoto wao na waliostahili wakakosa fursa hiyo. Hii ni tofauti na enzi za Mwalimu Julius Nyerere sisi tuliotoka familia maskini tuliweza kusoma hadi chuo kikuu bila matatizo. Cha msingi ni kuwa na sera nzuri inayoelekeza namna ya kuwapa fursa wasichana.

0 comments:
Post a Comment