Mwandishi Kenneth John Dar
Imebainika
kuwa tatizo la
upatikanaji wa huduma
bora za afya,
hususani kwa kinamama
wajawazito bado haziridhishi
kutokana na uchache
wa vifaa vya kujifungulia pamoja
na baadhi ya
wahudumu wa afya
(wakunga) kutokuwa na
lugha nzuri kwa
kinamama hao.
Wakizungumza
na mtandao wa
www,matukiodaima.com , kwa nyakati tofauti
wakazi wa jiji
la Dar es
salaam wamesema kuwa
ukiachana na changamoto
ya uchache wa
vifaa na vitanda
kwa baadhi ya
hospitali pia kinamama
wamekuwa wakikumbana na
kauli za kejeli
na matusi kutoka
kwa baadhi ya
wakunga swala ambalo
linaongeza uchungu zaidi
katika uzazi.
Annasemba Mhamba
ni miongoni mwa waliozungumza
na mtandao huu
na kusema kuwa
baadhi ya wakunga wengi
hujisahau na mara
nyingine hawajali kabisa
wagonjwa swala ambalo
ni hatari.
“Wakati mzazi
amefikia ule muda
wa kujifungua,lakini unakuta
wahudumu wa afya
hawapo karibu na
wewe ,hivyo unakuta mtu
amejifungua kabla hata
wakunga hawajafika”Alisema Annasemba
kwa hisia.
Aidha
naye Mama Nyemo
ambaye ni mkazi
wa Mbagala Chalambe
jijini humo, alisema
kuwa, shida kubwa
iliopo katika maeneo
mengi ni suala
la uwingi wa
watu ambao hauwiani na
idadi ya vituo
vya afya au
hospitali,jambo linalosababisha huduma
za afya kuwa
chini zaidi.
“Kwa mfano
kama sisi maeneo
ya Temeke, watu ni
wengi sana na
hospitali ambayo wanaitegemea
zaidi kwa maeneo
ya mbagala ni
hospitali ya Zakiem,unakuta wamama
wanatoka Mkulanga na
maeneo mengine wote
wanakwenda Zakiem,Sasa pale
wanapofika Zakiem huduma
wanapata lakini sehemu
ya kulala wagonjwa
ndio inakuwa ndogo”Alisema Mama
Nyemo.
Naye Rose
Elibariki Ntiliya, ambaye
ni muuguzi mkunga
katika hospitali ya
Dar Group, akijibu kuhusiana na taaluma yao
kutuhumiwa na watu
wengi kwa kutowajali kinamama
wajawazito, alikiri kuwepo
kwa baadhi ya
wauguzi wakunga wenye kutoa
maneno machafu kwa
kinamama wajawazito, Ingawaje alisema
swala hilo katika
hospitali yao haliko
kabisa na wala
hajawahi kusikia mtu akilalamikia
kuhusu lugha chafu.
Rose
aliwataka wauguzi wenye
tabia hiyo kuacha,
kwani si maadili
na si hivyo
walivyofunzwa darasani hata
katika taaluma zao .
“Kinachotakiwa hao
wauguzi kubadili tabia zao hizi
za kuwatukana kinamam,a
hasa walio leba katika
hali ya uchungu,na
kuwasaidia kwa hali
ya unyenyekevu na
hekima, kwa kufuata
maadili waliyofundishwa na
kuwasaidia mpaka mwisho
wa siku mama
ajifungue salama”Alisema Rose.
Sambamba
na hayo muuguzi
Rose aliwataka kinamama
kujenga tabia ya
kuhudhuria kliniki, ili
waweze kupata mafunzo
na maelezo jinsi
ya kuweza kujifungua
salama na kujua
afya zao pamoja
na mtoto aliye
tumboni, na hata waume
zao pia,jambo ambalo
litasaidia kuwafanya kujua
ni jinsi gani
watamlea mtoto wao.
Vile vile wakazi hao walitoa wito kwa serikali na mamlaka husika, kuhakikisha zinaongeza nguvu zaidi katika swala la uzazi, ili kufanya uzazi kutokuwa jambo hatari miongoni mwa wanajamii.
0 comments:
Post a Comment