RC Iringa Dr Christine Ishengoma |
Hawa ni wanaume waliofunga ndoa |
Hawa ni wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili (ukahaba)
...........................................................................................
SERIKALI ya mkoa wa Iringa imeagiza kuwepo kwa mkakati wa kuwasaka watu wanaume wanaojihusisha na biashara ya ushoga na wale wanawake wanaofanya shughuli za kuuza miili yao maarufu kama ukahaba.
Agizo hilo limetolea usiku huu katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Iringa kinachoendelea hadi sasa majira haya ya saa 1.59 usiku huu katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Hatua ya mkuu huyo wa mkoa kutoa agizo hilo imekuja baada ya mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa mbali ya kusikia kutoka majiji kama Dar es salaam na mengine hapa nchini kuwepo kwa biashara za ukahaba na ushoga ila uchunguzi unaonyesha mji wa Iringa ni miongoni mwa miji ambayo biashara hiyo ya ushoga na ukahaba inaendelea kukua kwa kasi na hivyo kutaka kuwepo kwa mkakati wa kupambana na biashara hiyo haramu.
" Ndugu wajumbe Manispaa ya Iringa ina watu wanaofanya biashara ya ushoga na ukahaba na mimi kama meya nina ushahidi wa kutosha ambapo idara inayohusika na viti dhidi ya UKIMWI Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wanaujua mtandao mzima wa biashara hiyo haramu"
Kutokana na ushahidi huo usio na shaka kutoka kwa meya Mwamwindi mkuu wa mkoa alilazimika kusimama na kuutaka mkoa kuweka mkakati wa kuwakusanya watu hao wote ili kuweza kuwasaidia kwa kuwapa miradi rafiki badala ya kuendelea na biashara hiyo haramu .
" Tusiwaache wapotee hawa ni watanzania wenzetu na yawezekana kuwakusanya na kuwapa elimu ili kuachana na shughuli hizo pia kuwapa miradi ya kufanya kwa ajili ya kuwaingizia kipato na sio kwa shughuli hiyo"
Mkuu huyo wa mkoa alisema wakati umefika kwa mkoa wa Iringa kuweka mkakati kabambe wa kupambana na madawa ya kulevya , ukahaba na ushoga katika mkoa huo.
0 comments:
Post a Comment