Wednesday, 29 January 2014

MFANYABIASHARA YA ULANZI IRINGA AANGUKA NA KUFA ENEO LA KITANZINI

Wananchi  wa Kitanzini  wakishuhudia  mwili wamarehemu huyo ukipakiwa katika   gari la polisi 

 Hii  ndio  Baiskeli iliyokuwa imebeba  Ulanzi kutoka  kijiji  ya Marehemu huyo ikiwa imeegeshwa klabuni ambapo alipaswa kuuza pombe hiyo
 Mama Mkwe wa marehemu huyo Bi Alophoncena Kunzugala  akiwa kando ya mwili wa mkwe wake kulia ,kushoto ni  polisi  waliofika  eneo la  tukio
 Mwili wa marehemu Erasto Ilomo aliyeanguka na kufariki dunia hivi punde
Mwili  huo  ukipakiwa katika gari la  polisi

MFANYABIASHARA   ya ulanzi kutoka  kijiji  cha Luhuhu Iheme kata ya Mgama Bw Erasto Ilomo ameanguka na  kufariki  dunia mara akiwa jirani kufika katika  Klabu  cha pombe za kienyeji eneo la Magari mabovu kata ya Miyomboni Kitanzini.


Tukio hilo  limetokea  majira ya saa5 asubuhi ya  leo  wakati  kijana  huyo akiwa amebakiza kama mita  15  kufika katika  klabu  cha pombe  kuwauzia pombe hiyo wateja  wake .


Wakizungumza na mtandao huu wa  www.matukiodaima.com eneo la  tukio baadhi ya  mashuhuda  ambao  hawakupenda  kuanika majina yao kwa kuhufu kusaidia polisi  walisema  kuwa kijana huyo alikuwa nyuma akiifuata Baiskeli yake ambayo  ilikuwa ikisukumwa na vijana  wawili   vibarua kutoka Ipogolo kama ilivyo siku zote .


Hata  hivyo kabla ya  kufika eneo la Klabu  hali  vijana hao  wakiwa  wameifikisha Baiskeli  hiyo  nje ya Klabu  wakisubiri  kupewa ujira wao kwa kazi ya  kusaidia kusukuma Baiskeli ndipo  walipoaona wananchi  wakimsaidia boss wao  huyo ambae alianguka ghafla .



Walisema  kuwa jitihada za wananchi  eneo hilo ambao ni wafanyabiashara  ziliweza kuonekana kwa kumnyanyua  kijana  huyo kutoka barabarani na kukalisha katika  ukuta wa nyumba ya jirani kabla ya  kuhema kwa nguvu mara tatu na kufariki dunia.


Mama Mkwe  wa marehemu huyo Alophoncena  Kunzugala  aliueleza mtandao   huu wa matukio daima kuwa hana hakika kama  mkwe  wake alikuwa mgonjwa kwani  hata jana  alifika mjini hapa kuleta  pombe hiyo.


Jeshi la  polisi mkoa wa Iringa  limethibitisha  kutokea kwa tukio hilo na  kuuchukua mwili huo kuupeleka katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku uchunguzi zaidi  ukiendelea.

0 comments: