Wednesday, 29 January 2014

CHAN 2014: MATUTA YAIFIKISHA LIBYA FAINALI SASA KUCHEZA NA MSHINDI GHANA AU NIGERIA!!


CHAN2014_LOGOLibya imetinga Fainali za CHAN 2014, Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao tu, baada ya kuitoa Zimbabwe kwa Mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia Sare ya 0-0 karika Dakika 120 za Mchezo huko Peter Mokaba Stadium, Polokwane Nchini Afrika Kusini.
Kwenye Robo Fainali, Libya pia ilishinda kwa Mikwaju ya Penati  baada kutoka 1-1 na Gabon katika Dakika 120 na kufuzu kwa Penati 4-2.
Leo hii, Libya, ambayo Fainali itacheza na Mshindi kati ya Ghana na Nigeria, ilifungana kwa Penati 3-3 na Zimbabwe baada Mikwaju Mitano na zikaja nyongeza za Penati moja moja na kila Timu ikakosa mbili na Libya kuibuka kidedea kwa Penati 5-4.
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Cape Town Stadium]
Morocco 3 Nigeria 4 [3-3 baada Dakika 90]
Mali 1 Zimbabwe 2
Jumapili Januari 26
[SAA za Bongo]
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
Ghana 1 Congo DR 0
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
[SAA za Bongo]
Zimbabwe 0 Libya 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 5-4]
2130 Ghana v Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
[SAA za Bongo]
1800 Zimbabwe v Ghana/Nigeria [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]
Libya v Ghana/Nigeria

0 comments: