Vijana wawili wachoma nyama katika eneo la mtaa wa M.R katika Manispaa ya Iringa wamechomana kisu shingoni kutokana na ugomvi wa zamu katika kazi hiyo.
Tukio hilo la kushangaza limetokea leo mida ya mchana wakati kijana anayetambulika kwa jina la Fadhil kujikuta akichomwa kisu na mwenzake John Shirima ambae ndie alikuwa akiingia kazini .
Imedaiwa kuwa vijana hao walikuwa wakipokezana eneo la kazi na kwa kawaida baada ya kupokezana yule anayepokelewa anapaswa kuondoka jikoni na kuachia jiko wazi ila kwa leo Fadhil hakuweza kuondoka na badala yake aliendelea kuganda jikoni hali iliyopelekea John kuchukua kisu na kumchoma kisu mwenzake.
Hata hivyo wakati akijaribu kukimbia baada ya kumchoma kisu mwenzake shingoni aliweza kukimbia kabla ya kukamatwa na kufikishwa polisi huku majeruhi aliyechomwa kisu shingoni akikimbizwa Hospital .
picha na undani wa tukio hili utaendelea kuzipata hapa
0 comments:
Post a Comment