Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Kwani amesema jitihada zinazofanywa na NHIF katika mkoa wa Iringa ni kubwa na kuiwezesha wilaya ya Kilolo kuendelea kufanya vizuri katika mfuko huo na hivyo kuomba mfuko kuboresha Hospital hiyo ya wilaya ili kuepusha wajawazito kuendelea kupoteza maisha kwa kukosa huduma bora za afya.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa, Emmanuel Mwikwabe akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mfuko huo mkoa wa Iringa alisema kuwa kuna haja ya kuunda tume maalum ya kuchunguza dawa katika Hospital na vituo vya afya kwani ukifanya uchunguzi utabaini kuwepo kwa matumizi yasiyo mazuri ya dawa hizo.
Alisema kuwa changamoto za mfuko huo na ule wa CHF au TIKA katika mkoa wa Iringa ni pamoja na Halmashauri kushindwa kuwasilisha maombi ya Tsh milioni 96.6 kwa ajili ya malipo ya tele kwa tele na hivyo kukwamisha wanachama wake kunufaika na mifuko hiyo.
Pia suala la usimamizi mbaya wa fedha za uchangiaji wa huduma za matibabu (NHIF na CHF ) badala ya fedha zitokanazo na NHIF na CHF kutumika kuboresha huduma za matibabu zinazotumika katika shughuli ambazo ziko nje ya miongozo ya matumizi ya fedha za uchangiaji.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa, Emmanuel Mwikwabe akitoa taarifa za mfuko huo leo katika kikao cha RCC
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alitoa muda wa miezi mitatu kwa Halmashauri ambazo hazijapeleka fedha hizo kuhakikisha zinafanya hizo ndani ya miezi mitatu ijayo.
0 comments:
Post a Comment