Wednesday, 29 January 2014

UKOSEFU WA VYOO WASABABISHA WANAFUNZI ZAIDI YA 300 KUJISAIDIA VICHAKANI


images
 Na Gladness Mushiwa  -Arusha
ZAIDI ya wanafunzi 300 kutoka katika shule ya msingi Engatani iliopo
Kata ya MakibaWilayani Meru Mkoani Arusha wapo hatarini kupata

magonjwa ya mlipuko kutokana na kuwa shule hiyo haina vyoo na hivyo

wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kujisaidia kwenye vichaka.
Aidha tatizo hilo la ukosefu wa vyoo katika shule hiyo umedumu kwa
miaka miwili sasa mara baada ya mvua kubwa kufukia matundu ya vyoo

katika shule hiyo.
Akiongea na “Fullshangwe” shuleni hapo mapema jana Mkuu wa shule hiyo Adamu
Kapaya alisema kuwa shule hiyo haina vyoo kabisa na hivyo wanafunzi

wanapojisikia kujisaidia wanalazmika kwenda kwenye vichaka au kwenye

mazingira ambayo yamejificha kwaajili ya kuweza kujisaidia
Alidai tatizo hilo limeanza mwaka 2012 ambapo mvua kubwa ya masika
ilionyesha iliweza kuziba matundu ya vyoo na hivyo kusababisha kutitia

kwa vyoo hivyo na mpaka sasa hakuna huduma ya vyoo hali ambayo

imesababisha madhara makubwa sana kutokea katika shule hiyo.
“baada ya kuona kuwa mvua zimesababisha shule yetu kukosa vyoo
niliandika barua kwa mkurugenzi ambapo naye alihaidi kushugulikia

tatizo hili na kwa uongozi wa serikali ya kijiji nlakini mpaka sasa

hali ndio kama hii hakuna choo wanafunzi wanakimbilia zaidi kwenye

Vichaka”alisema Adamu
Pia aliongeza kutokana na hali hiyo imesababisha hata mazingira ya
shule kuwa machafu sana pamoja na kuwepo kwa hewa chafu kutokana na

vinyesi ambavyo vimezagaa kwenye mazingira ya shule hiyo na pembezoni

mwa shule hiyo hivyo jitiada za haraka sana zinatakiwa kufanyika
Awali diwani Viti maalumu wa Kata hiyo ya Makiba.Bi Joycye Odoko
alisema kuwa ukosefu wa choo kwenye shule hiyo umesababishwa na baadhi

ya watendaji kukwepa kuombea bajeti shule hiyo kwa lkuwa ipo mpakani

mwa wilaya ya Meru hali ambayo inasababisha wanafunzi waishi mazingira

magumu sana
Bi Joyce amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi katika eneo hilo ni
wafugaaji lakini hawana uwezo kitu ambacho kama wangekuwa na uwezo

basi wangeweza kuwasaidia wanafunzi hao
“wananchi wa hapa hawana uwezo ingawaje kwa sasa wameshaweka utartibu
hata wa kukusanya mawe , na mchanga ili kuuanza rasmi zoezi hilo

japokuwa bado hawataaweza kujenga mpaka kumalizika kwa matundu ya vyoo

sassa tunaomba kuwepo  naushirikiano madhubuti baina yetu sisi

viongozi ili tuweze kuwasaidia wanafunzi hawa kwani wapo kwwenye

hatari kubwa sana ya kuweza kupata magonjwa ya mlipuko hasa

kipindupindu”aliongeza Jocye
Akiongelea sakata hilo kwenye baraza la madiwani wa halmahauri ya Meru
Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye Goodson Majola alisema kuwa kwa sasa

bajeti ya Halmashauri hiyo imelenga kutatua sehemu mbalimbali zenye

kero na hivyo pindi watakapopata fedha kutoka Serikali kuu basi

wataweza kutatua changamoto mbalimbali

0 comments: