Baadhi
ya wakazi wa mji wa Singida,wakipokea helkopta iliyombeba mwanasheria
wa CHADEMA, Tundu Lissu,ambaye alihutubia kwenye uwanja wa Ukombozi
mjini Singida.
Mwanasheria
wa CHADEMA Tundu Lissu,akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Singida
katika operation ya kuimarisha chama hicho.Mkutano huo ulifanyika katika
uwanja vya Ukombozi mjini Singida.
Baadhi
wa wakazi wa Singida mjini,wakimsikiliza mwanasheria wa CHADEMA Tundu
Lissu, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa Ukombozi mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MWENYEKITI wa Baraza la
Vijana Taifa (BAVITA), John Heche amesema Chadema kitaendelea kuwavua
uanachama kiongozi au mwanachama yeyote, pindi anapobainika kusaliti
ustawi wa chama hicho.
Heche aliyasema hayo hivi
karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa ukombozi mjini hapa.
Amesema CHADEMA kamwe
haitawalea wasaliti kama CCM ambayo inalea mafisadi na mawaziri
mizigo,itaendelea kuwavua uanachama wasaliti bila kujali umaarufu wa mtu
au kiongozi.
“Kelele zimepingwa sana
kwamba CHADEMA sasa kinakufa kisa eti Zitto Kabwe,amevuliwa nafasi zake
zote za uongozi.Wanasingida,hivi kweli CHADEMA ife kwa sababu ya mtu
mmoja tu.Haitatokea kabisa”,amesema na kuongeza;
“Viongozi wote mashuhuri
hivi sasa kwenye chama cha CHADEMA,hata wakiondoka,chama kitabaki pale
pale na hakitaterereka.Hakuna kiongozi au mwanachama ambaye yupo juu ya
CHADEMA,kwa hiyo sisi viongozi tutaondoka,lakini CHADEMA itabaki pale
pale”,alisisitiza Mwenyekiti huyo.
Heche amesema CHADEMA
ikichukua dola,haitawalinda mafisadi au viongozi mizigo kama inavyofanya
CCM,CHADEMA itawafukizia mbali na endapo kutakuwa na adhabu ya
kuwanyonga hadi wafe,adhabu hiyo itatekelezwa bila ubishi.
Kwa upande wake Mwanasheria
wa CHADEMA,Tundu Lissu amewataka Watanzania mwakani (2015),kuchagua
rais mwadilifu na sio anayehonga mapadre fedha chafu zilizotokana na
ufisadi.
Akifafanua,amesema baadhi
ya viongozi hivi sasa wanapita kwenye nyumba za ibada kutoa rushwa na
kudai kwamba zamu yao ya kuwa rais,imewadia.
“Watanzania
wenzangu,kiongozi au mtu ye yote anayetaka urasi kwa kuhonga fedha za
ufisadi huyo hatufai tunataka raisi ajaye awe ni mtu mwadilifu na mwenye
uchungu wa kweli na Tanzania”,amesema Tundu.
0 comments:
Post a Comment