Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na
Usalama, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa
watu walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja
na kusimamia ujenzi wa nyumba za muda wa waathirika hao.
Rais pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako waathirika hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.
Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia waathirika wa mafuriko hayo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia huduma zote za

msingi ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza kujitegemea tena.
Rais Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea kambi za waathirika wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.
Katika hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo waathirika hao wanalala, Rais Kikwete amesema ameagiza Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.
“Kazi yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”
Kuhusu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha na hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini na waje kupata vichomi.”
Kuhusu maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye makambi.
Rais ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.
“Hili ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”

KUTOKA KWA MWANDISHI MWINGINE...
Katika mkutano huo pia rais Kikwete amewataka Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kufanya kazi za kuwahudumia wananchi, katika nyakati za matatizo.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo, baada ya kutoridhishwa na takwimu za waathirika wa mafuriko zilizotolewa na Uongozi wa Mkoa kuhusu idadi ya kaya na watu waliokubwa na mafuriko katika Tarafa ya Magole, wilaya ya Kilosa, Dakawa wilaya ya Mvomero na Gairo kutoonesha mchanganuo halisia.
Rais Kikwete alisema hayo wakati wakiwahutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Magole, Tarafa ya Magole, wilayani Kilosa eneo la viwanja vya Shule ya Sekondari Magole, ambapo kumewekwa Kambi ya muda kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu.
Rais Kikwete aliwasili leo mchana kwa usafiri wa helkopta ya Polisi na kabla kuwahutubia wananchi alitembelea daraja lililoathirika na mafuriko na baadaye kupanda tena Helkopta kwenda kujionea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko na kupewa taarifa ya athari ya mafuriko kwa za Kata za wilaya ya Kilosa, Gairo na Mvomero.
Kutokana na kasoro hizo, Rais alitoa siku moja ya kwa Mkuu wa Wilaya na Mkoa wampatie takwimu kamili zikiwa na majina ya watu waliobomolewa nyumba kuishi kwa majirani na katika makambi ili misaada inayotolewa iwafikie walengwa na si wajanja wachache ambao si walengwa.
“ Uongozi unapimwa katika kipindi cha matatizo ya watu , hivyo sijaridhika na takwimu hizi, haioneshi walengwa halisia...hivyo jipangeni vizuri inape taarifa kamili kesho ili Waziri William Lukuvi na wengine wazifanyie kazi kuwezesha upatikanaji wa huduma bila kuanchwa mtu aliyeathiwa na mafuriko” alisisitiza.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akisoma takwimu za waathirika wa mafuriko katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Kilosa, Mvomero na Gairo, alisema jumla ya watu 12,472 walikumbwa na mafuriko hayo.
Pia alisema ,kaya 2,759 zimeathiriwa , wakati nyumba 1,141 zilibomolewa na nyumba 2,922 kuzungukwa na maji na kuhitajika tani 635.5 za chakula kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na kiasi cha sh: milioni 57 kwa ajili ya kujenga makazi ya muda.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Dk Godfrey Mtei, alimjulisha Rais kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Bohari kuu ya dawa (MSD) imetoa dawa za aina mbalimbali na vifaa tiba na magodoro vyenye thamani ya sh: million 80 .
Pia alisema , kutokana na athari za mafuriko hayo, watu 300 walijitokeza kupatiwa dawa katika kituo cha muda cha matibabu kilichipo eneo la Kambi shule ya Sekondari Magole na kwamba wanaendelea kuthibiti magonjwa ya mlipuko.
Wakati huo huo rais Kikwete, ameagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) kufika Kijiji cha Magole kwa ajili ya kujenga kambi za muda za mahema na mabati ili kuwawezesha waathirika wote ambao wamekubwa na mafuriko hayo na hawana nyumba za kuishi waweza kuishi kwenye kambi hizo.
“ Mafuriko haya ni makubwa na hayajawahi kutokea , watu wameathiriwa kwa nyumba zao kubomoka, kujaa maji na kuwafanya kukosa makazi na wengi wao wanalala chini “ alisema Rais Kikwete mbele ya wananchi.
Hivyo alisema kutokana na idadi kubwa ya waathirika kulala chini kwa kukosa makazi na madogoro, Rais alisema kuwa, Serikali yake inawaomba wenye viwanda binafsi vya kutengeneza magodoro waliyonayo waiuzie Serikali kwa njia ya mkopo ili iweza kuwagawia waathirika hao.
Kwa upande wa Chakula, alisema Serikali inacho chakula cha kutosha kwenye maghala yake, hivyo itayafungua kwa kuwasambazia chakula wananchi ambao wameathirika na mafuriko hayo hususani Mahindi na Maharage na pia kuwataka wadau wengine wajitokeze kusaidia kutoa chakula hasa mchele.
Kuhusu huduma ya maji, alisema, itaendelea kutolewa na magari ya Jeshi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wenzetu wa kichina hadi pale huduma ya maji kwenye Kijiji hicho na vingine itakapotengemaaa.
0 comments:
Post a Comment