Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda
(Mb) anatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014
akitokea Geneva, Uswisi alikoenda kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati
ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015. Kamati hiyo inayoundwa na Maspika
37 walioteuliwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana
tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge
Duniani Mjini Geneva. Mkutano wa pili wa Kamati hiyo ya Maandalizi
utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha,
kabla ya kwenda Geneva, Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika
wa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika
Wellington, New Zealand kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2014.
Kwa
ujumla, ushiriki wa nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri
ya kuitangaza na kuipa heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa
jukwaa madhubuti linalotumika kuiweka nchi katika ramani ya dunia na
kuonyesha vivutio hususan katika nyanja za uwekezaji, utalii na
maliasili pamoja na fursa mbalimbali zilizomo.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
28 Januari 2014
0 comments:
Post a Comment