Jeshi la polisi
kanda maalum Dar
es salaam limetangaza
kuanza rasmi mpango
wa kupunguza ajali
za pikipiki barabarani,
kwa kuhakikisha madereva
wote wa bodaboda
wanafuata sheria na
taratibu za kutumia
vyombo hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa
habari jijini Dar
es salaam, kamishina
wa polisi kanda
maalum ya Dar
es salaam CP
Suleiman Kova alisema
kuwa uamuzi huo
umekuja baada ya
kufanya uchunguzi, na
kugundua ajali nyingi
za bodaboda zinatokana
madereva wengi wa
piki piki kutokuwa
na elimu ya
usalama barabarani,pia baadhi
yao hawafuati sheria
ikiwa ni pamoja
na kuvaa kofia
ngumu pindi wanapotumia
vyombo hivyo.
Aidha
kamanda Kova alibainisha
sifa ambazo mtumiaji
wa piki piki
atatakiwa kuwa nazo
kila atumiapo chombo
hicho, ambazo ni
pamoja na kuvaa
kofia ngumu dereva
pamoja na abiria
wake,kutopakia abiria zaidi
ya mmoja maarufu
kama mshikaki,kuwa na
leseni ya kuendeshea
piki piki , na pia
mtumiaji atatakiwa
kuwa na bima
itakayomsaidia endapo atapata
ajali.Pamoja na hayo
Kova aliendelea kusema
kuwa sifa nyinginezo
ni lazima piki
piki iwe na
sifa za kutembea
barabarani.
“Boda boda
lazima zifuate sheria
na taratibu za
nchi kwani bila
ya hivyo mwisho
wa siku hilo
ni bomu,sisi hatukatai
wao kufanya kazi,
kazi wafanye ila wafuate
sheria sheria”Alisisitiza kamanda
Kova.
Vile
vile kamanda Kova
amesema kuwa kuanzia
sasa ni marufuku
kwa boda boda kupaki
piki piki mbele ya
benki au
karibu na benki,
kwani jambo hilo
linahatarisha usalama wa
taasisi hizo za
kifedha, na kuwaomba
halmashauri wa jiji
la Dar es
salaam kuwasaidia kuainisha
maegesho maalum kwa
ajili ya piki
piki.
Na
katika hatua nyingine
jeshi la polisi
kanda maalum limefanikiwa
kumkamata mtuhumiwa Grace
Adrew Chapanga (34),
ambaye ni mama
wa nyumbani ,mkazi wa
Bunju “B” jijini
Dar es salaam
kwa kosa la
wizi wa mtoto
mchanga wa kike , mwenye
umri wa mwezi
mmoja aitwaye Veis
Venus aliyeibwa Desemba
27 ,2013 maeneo ya
mwenge jijini Dar
es salaam.
Taarifa
zinasema kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa baada
ya kumhadaa mama
wa mtoto aitwaye
Salma Frank (29) ,
mkazi wa
kawe Mji mpya
kwa kumwomba ambebe
huku wote wakiwa
abiria wa daladala
wakitokea hospitali ya
mwananyamala .
Lakini
walipofika Mwenge kituo
cha daladala mtuhumiwa
aliteremka upesi na
kutoweka na mtoto,pindi
mwenye mtoto akikusanya
vitu vingine alivyokuwa
navyo.
Mtuhumiwa
huyo alitenda kosa
hilo kwa kushirikiana
na Halima Haufi
Alabi, (46) , mkazi wa
Boko maliasili ambaye
naye alikamatwa januari
4,2014.Watuhumiwa wote wawili
baada ya kutenda
kosa hilo waliondoka na
kuelekea Sumbawanga mkoani
Rukwa , ambapo Grace Adrew
Chapanga alimdanganya mumewe
kuwa yeye ni
mjamzito na angependa
kwenda kujifungulia nyumbani
kwao huko Sumbawanga.
Aidha
upelelezi wa tukio
hilo ulifanikiwa kumkamata
mume wa Grace
Adrew Chapanga aitwaye Daniel
James Mwaikambo (38),
ambaye ni mkazi
wa bunju “B”
na ni mfanyakazi
wa uhamiaji makao
makuu Dar es
salaam, na ndipo
wakaenda naye hadi
Sumbawanga ambapo walimkuta
mtuhumiwa na kumkamata
Awali
taarifa zinasema kuwa , tangu
wafunge ndoa mwaka
2010 , wawili hao hawajabahatika kupata
mtoto.
Lakini mnamo mwaka
2012 Grace Adrew
Chapanga alifanyiwa upasuaji
wa uvimbe tumboni
,ambapo Daktari alimwambia
hatoweza kushika mimba
tena jambo ambalo
Grace hakumweleza mume
wake , wala ndugu yake
yoyote , hadi alipopanga njama
na hatimaye kufanikiwa
kumuiba mtoto huyo.
Hata hivyo taarifa ya jeshi la polis kanda maalum inasema kuwa, upelelezi juu ya tukio hili unaendelea kwa kufuatilia uchunguzi wa vinasaba (DNA) vya mama mzazi na mtoto aliyeibwa.Pia mtoto amekabidhiwa kwa mama yake mzazi.
0 comments:
Post a Comment