Zipo habari nzito zimeibuka kuwa Kiungo
wa Germany, Toni Kroos, yupo tayari kuihama Bayern Munich baada
kuvunjika Mazungumzo na Klabu hiyo kuhusu kuboresha Mkataba wake na hili
limetoa mwanya kwa Klabu nyingine kumyemelea huku Bayern ikiwa tayari
kumuuza ikiwa Dau litafika Pauni Milioni 25.
Toni Kroos amekuwa akiitaka Bayern
imlipe Mshahara sawa na Mastaa wengine kama kina Franck Ribbery na madai
yake ni kulipwa Pauni 150,000 kwa Wiki ambazo Bayern inatia ngumu
kumlipa lakini Manchester United imejitokeza kuwa tayari kumlipa.
Ijumaa iliyopita Meneja wa Man United,
David Moyes, alikwenda kumtazama Kroos akiichezea Bayern ilipoifunga
Borussia Moenchengladbach 2-0 na kukaribshwa Uwanjani na Wakala wa
Kroos, Sascha Breese, na pia kukaa pamoja nae huku wakiongea kwenye
Mechi hiyo.
Mkataba wa Kroos na Bayern unamalizika
mwishoni mwa Msimu ujao na Mtendaji Mkuu wa Bayern, Karl-Heinz
Rummenigge, amekiri kukwama kwa Mazungumzo ya Mkataba mpya kwa vile
hawawezi kukidhi matakwa ya Staa huyo wa Germany kwa kuhofia kuleta
machafuko miongoni mwa Wachezaji wao kuhusu Vipato.
0 comments:
Post a Comment