Thursday, 30 January 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
DSC00207 ·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
·         AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
·         AJALI YA GARI NA PIKIPIKI KUGONGANA HUKO VWAWA MKOANI MBEYA NA KUSABABISHA VIFO.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
MNAMO TAREHE 29.01.2014 MAJIRA YA SAA 07:30HRS HUKO KAYUTI WILAYANI RUNGWE TRACTOR LENYE NAMBA ZA USAJILI T.409 BNN LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA AMASHA SAMSON (28) MKAZI WA KAYUTI LILIGONGANA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.667 PCE AINA YA BOXER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA LUSAJO MWAKAMBA (30) MKAZI WA KYELA NA KISHA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA WA PIKIPIKI AITWAYE ALFA MNDENDEMI (24) MKAZI WA MKOANI NJOMBE MUDA MFUPI WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU NA MAJERAHA KWA DEREVA WA PIKIPIKI HIYO . UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDESHA TRACTOR ALIKATISHA BARABARA GHAFLA KUTOKA KUSHOTO KWENDA KULIA BILA KUCHUKUA TAHADHALI YOYOTE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA WA TRACTOR AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.433 ATP AINA YA MITSUBISHI CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA LILIACHA NJIA KISHA KUPINDUKA HUKO KATIKA ENEO LA NAMBA ONE WILAYANI RUNGE NA KUSABABISHA KIFO KWA ANANGISYE STEWAT (27) TINGO NA MKAZI WA IKUTI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRAYA SAA 19:30HRS NA UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHAKE NI BAADA YA DEREVA WA GARI HILO KUPITIWA NA USINGIZI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI/RAIA MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE. 
AJALI YA GARI NA PIKIPIKI KUGONGANA HUKO VWAWA MKOANI MBEYA NA KUSABABISHA VIFO.
KATIKA AJALI NYINGINE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.784 AVB AINA YA TOYOTA COASTER MALI YA ILASI SEKONDARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA GODFREY MWALINGO (56) MKAZI WA ICHENJEZYA LILIGONGANA KATIKA ENEO LA ICHENJEZYA WILAYANI MBOZI NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.268 CTR AINA YA KING LION ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA HARUNA JACOB (25) NA KUSABABISHA VIFO KWA DEREVA HUYO WA PIKIPIKI NA ABIRIA WAKE AITWAYE KELVIN JACOB (21) WOTE WAKAZI WA ISANGU. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRA YA SAA 07:30HRS ASUBUHI NA CHANZO CHAKE NI MWENDO KASI WA WA PIKIPIKI, DEREVA AMEKAMATWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI UNAUA NA NI HATARI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments: