>>VIINGILIO: KUANZIA 5,000/=
>>JUMAPILI: YANGA v MBEYA CITY, AZAM v KAGERA SUGAR!
>> SERENGETI BOYS YAPANGIWA AFRIKA KUSINI, KOMBE LA AFRIKA!
>> TFF MPYA YATIMIZA SIKU 100
>> BODI YA LIGI YAZIPIGA JEKI KLABU ZA FDL!
SOMA ZAIDI:
Release No. 015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 31, 2014
SIMBA YAIKARIBISHA OLJORO JKT DAR
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi hii kwa mechi nne
ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo
itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000, sh. 15,000 na
sh. 20,000 kwa VIP A. Refa atakuwa Nathan Lazaro kutoka mkoani
Kilimanjaro wakati Kamishna ni Hakim Byemba wa Dodoma.
Uwanja wa Azam uliopo Mbagala siku hiyo
kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti United na Mgambo Shooting
kutoka Handeni mkoani Tanga kwa viingilio vya sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Jumapili (Februari 2 mwaka huu) ni Yanga
vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni), na
Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 10 kamili
jioni).
Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5
mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania Prisons vs Coastal Union (Uwanja
wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi).
SERENGETI BOYS YAPANGIWA AFRIKA KUSINI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini
ya miaka 17 (Serengeti Boys) itacheza na Afrika Kusini katika mechi za
mchujo kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa umri huo
zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Serengeti Boys ambayo pamoja na nchi
nyingine 17 zimeingia moja kwa moja katika raundi ya pili itaanzia mechi
hiyo nyumbani kati ya Julai 18-20 mwaka huu wakati ile ya marudiano
itafanyika nchini Afrika Kusini kati ya Agosti 1-3 mwaka huu.
Ikifanikiwa kuitoa Afrika Kusini,
Serengeti Boys itacheza mechi ya raundi ya tatu na ya mwisho na mshindi
wa mechi kati ya Misri/Sudan vs Congo Brazzaville.
Nchi nyingine ambazo zimeingia moja kwa
moja raundi ya pili ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Botswana, Burkina
Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali,
Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kutangaza benchi la ufundi litakaloiongoza Serengeti Boys hivi karibuni.
TFF MPYA YATIMIZA SIKU 100
Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, Februari 4
mwaka huu inatimiza siku 100 tangu iingie madarakani katika uchaguzi
uliofanyika Oktoba 28 mwaka jana.
Hivyo, Rais Malinzi atazungumza na
waandishi wa habari Februari 7 mwaka huu kuelezea utekelezaji wa Ilani
yake ya uchaguzi. Muda na mahali utakapofanyika mkutano huo mtaarifiwa
baadaye.
BODI YA LIGI YAZIPIGA JEKI KLABU ZA FDL
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa
katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam
ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye akaunti za klabu husika.
Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB zinatakiwa
kuwasilisha haraka.
Klabu za FDL ni African Lyon, Burkina
Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa JKT, Kimondo, Kurugenzi
Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na Mwadui.
Nyingine ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es
Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro, Polisi Tabora,
Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment