Monday, 27 January 2014

RAIS WA BARCA, JOSEP MARIA BARTOMEU: ‘MESSI HAUZWI NG’OO!!!’

>>PSG YAMNYATIA!!

>> SKANDALI LA UHAMISHO NEYMAR: MWANACHAMA HAFUTI KESI HADI…..!!
LIONEL_MESSISUPASTAA wa Barcelona Lionel Messi hatauzwa na Klabu ipo mbioni kujadiliana nae kuhusu Mkataba mpya kwa mujibu wa taarifa ya Rais mpya wa Klabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Huku ikiripotiwa kuwa Paris St-Germain ilikuwa ikimnyemelea Messi, mwenye Miaka 26, Rais wa muda wa Barca, Bartomeu, amedai: “Klabu itakaa chini na kujadiliana Mkataba mpya. Tutafanya kila tuwezalo abaki awe Mchezaji anaelipwa vizuri sana.”

Messi na Goli:
-Msimu huu, Messi ametoa Msaada wa Magoli mara 36 na kufunga Bao 18.

Msimu uliopita, Messi alifunga Bao 60 katika Mechi 50 lakini Msimu huu amekuwa akisuasua kwa kufunga Bao 18, 8 zikiwa kwenye La Liga, na pi kuumia na kuwa nje kwa Miezi miwili.
SKANDALI LA UHAMISHO NEYMAR: MWANACHAMA HAFUTI KESI HADI…..!!
Wakati huo huo, Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ndie aliefumua Skandali la Uhamisho wa Neymar uliofanfa Rais wa Barcelona, Sandro Rosell, ajiuzulu na Kesi kutinga Mahakamani kwa uchunguzi juu ya Ubadhirifu wa Fedha kuhusu Uhamisho huo, amesema hatafuta Kesi hadi apewe kimaandishi uhakika kwamba Barca haitalipa kisasi kwa kumdai Fidia.
Kufuatia kujiuzulu kwa Sandro kulikuwa na dhana kuwa Kesi hiyo itafutwa ingawa Wakala wa Cases alidokeza kuwa hilo linawezekana.
Cases mwenyewe amethibitisha kuwa Rais wa muda wa Barca, Josep Maria Bartomeu, amemhakikishia Klabu haitamchukulia hatua yeyote, lakini Mwanachama huyo anataka Msimamo huo uwe wa Kimaandishi.
Hata hivyo, hadi sasa haijulikani ikiwa Cases ataamua kufuta Kesi kama Mahakama itakubali kuacha uchunguzi wake wa Ubadhirifu wa Fedha ambao ukithibitika ni Kosa la Jinai.

0 comments: