Morsi amesisitiza kuwa yeye ni Rais na hata kuhoji uhalali wa mahakama
Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed
Morsi, ameonyesha ukaidi katika siku yake ya kwanza katika mahakama
nchini Misri, kujibu tuhuma za njama ya kuwatorosha wafungwa kutoka jela
wakati wa mapinduzi ya kiraia ya Hosni Mubarak 2011
Morsi aliyefikishwa mahakamani na washitakiwa
wenzake, alihoji uhalali wa mahakama hiyo na kusisitiza kuwa yeye bado
ni rais halali wa nchi hiyo.
Kesi dhidi ya Morsi imeahirishwa hadi Februari.
Zaidi ya washitakiwa wengine 130 wakiwemo viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood wameshitakiwa pamoja na Morsi.
Bwana Morsi hajakuwa huru tangia jeshi limuondoe madarakani mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kama rais.
Wakati huohuo, wizara ya mambo ya ndani imesema
kuwa afisaa mmoja wa wizara hiyo Generali Mohammed Saeed, alipigwa
risasi akielekea kazini.
Mauaji hayo yanatokea wakati mashambulizi dhidi
ya maafisa wa usalama katika siku za hivi karibuni na masaa kadhaa baada
ya jeshi kumuunga mkono mkuu wake Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi
kugombea urais.
Hali ya usalama imeimarishwa nje ya ya jengo la wizara hiyo , lakini hakuna hata mfuasi mmoja wa Mohammed Morsi amejitokeza.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood, limeharamishwa
na kutajwa kama kundi la kigaidi na pia wameifanya hatia uungwaji mkono
wa kundi hilo.
Makabiliano kati ya wafuasi wa Brotherhood pamoja na vikosi vya usalama, yaliripotiwa kutokea katika eneo la Ramses mjini Cairo.
Morsi anatuhumiwa kwa kosa la kupanga njama ya
kuwatorosha wafungwa kutoka katika gereza la Wadi al-Natrun wakati wa
ghasia za mwaka 2011.
Mara ya kwanza alipofikishwa mahakamani mwezi
Novemba, Morsi alikataa kutambua uhalali wa mahakama wala kuvalia vazi
la gerezani.
0 comments:
Post a Comment