Monday, 27 January 2014

KUMBE: GADDAFI ALIBAKA WATOTO WA MIAKA 14 WAKIKE NA WAKIUME KWENYE CHUMBA MAALUM

article-2545819-1AF574EA00000578-367_636x382 
.Kanali Gaddafi alikuwa na vyumba maalum kwa wafungwa wa ngono kwenye majumba yake
.Mamia ya vijana wasichana kwa wavulana walikuwa watumwa wa ngono kwake
.Dikteta huyo alitembelea shule na kuchagua vigoli ‘bikira’ wa kufanya nao ngono
.Aliuawa mwezi Oktoba 2011 baada ya miaka 42 ya udikteta
Na Damas Makangale,  Kwa Msaada wa Mtandao

IMETIMIA zaidi ya miaka miwili tangu kukamatwa na baadaye kifo cha Muammar Gaddafi, dikteta wa Libya ambaye utawala wake wa miongo kadhaa ulikabiliwa na umasikini mkubwa vitisho, mauaji ya kikatili kwa raia wasio na hatia na ugaidi.
Wakati kiongozi huyo wa zamani anatolewa nje baada ya kuanguka kwenye mtaro wa maji machafu baada ya kupigwa risasi kati kati Oktoba 2011, kifo chake na damu yake kilimaliza vita ya NATO ya wenyewe kwa wenyewe na alikuwa amevuruga nchi tangu mwanzo wa mwaka huo.
Maisha yake ya kikatili yamekuwa kama sehemu ya Walibya wengi na pole pole baadhi ya watu kutoka kwenye kabila lake wana visasi na wanaendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza mara kwa mara kwenye baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
article-2545819-1AF2E72900000578-769_634x549
Udhalilishaji: Hii ni kifaa kikamilifu maalum kama aina ya kitanda chenye uwezo wa kuangalia magonjwa ya zinaa kwa wasichana wadogo kabla ya kupelekwa kwa Dikteta Gaddafi kwa sughuli ya ngono.
Lakini sasa kwa upande mwingine baadhi ya wasichana na wavulana waliofanyiwa unyama na unyanyasi wa kijinsia wana uchungu na waliofanyiwa ndani ya miaka 42 ya utawala wake kwa sababu walipigwa, kubakwa na kulazimishwa kuwa watumwa wa ngono kwa kwake.
Taarifa zinasema wengi walikuwa na wasichana waliotekwa nyara kutoka shule za sekondari na vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Tripoli na walikuwa wanapokea maagizo kutoka kwa wasaidizi wa karibu wa Kanali Gaddafi kuwapeleka katika moja ya vyumba maalumu vya ngono.
Wengi wa wasichana waliobakwa na Kanali Gaddafi walikuwa na mabikira na wanafunzi wa vyuo vikuu walipimwa kwanza magonjwa ya zinaa (STD) na kisha kupelekwa katika moja ya vyumba maalum kwa kazi ya ngono.
Katika kipindi cha miezi 26 tangu aondolewe madarakani, sehemu za ngono au mapango ya Gaddafi ambayo yeye mara kwa mara kubaka wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 ilibakia imefungwa. Lakini leo mambo ya ndani ya sehemu za ngono za dikteta huyo katili inaweza kuonekana kwa mara ya kwanza katika picha za mtandao wa BBC4 documentary.
article-2545819-1AF2E73100000578-385_634x422
Makubwa hiki ni chumba cha kulala katika moja ya vyumba vya ngono vya Kanali Gaddafi ambapo kuna kuta za kahawia na kitanda cha kisasa viwili ambavyo kutumia kufanya ngono na wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 na kuwanyanyasa kingono.
Ndani ya mapango hayo wasichana walilazimishwa kuangalia picha za uchi ili kuwafanya wawe na hamu na ushawishi wa kufanya naye ngono kati kati ya mikono katili ya Gaddafi.
Wakati wa mauaji yake kundi la vijana baada ya kushuhudia Kanali Gaddafi akidondoka katika ya mitaro ya barabara baada ya kupigwa risasi katika kichwa na kuanza kuburuzwa ovyo barabara kisha kuuwawa kinyama.
Mwalimu mmoja wa shule Tripoli alikumbuka jinsi wasichana wote walikuwa wa wadogo sana. Baadhi walikuwa na umri wa miaka 14 tu, “amesema. ‘Wao walikuwa wanachukua tu wasichana wadogo wakitaka na hakuna huruma ilikuwa ni maisha ya kuogopesha sana,” amesema mwalimu huyo.
article-2545819-1AF2E73500000578-574_634x512
Baadhi ya walinzi waliokuwa wakimlinda Gaddafi ambao nao walitoa rushwa ya Ngono kupata kazi.
Mama mmoja ambaye binti yake alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tripoli, anasema kwamba wanafunzi walikuwa na hofu mara tu ikitangazwa kwamba kanali Gaddafi anakuja kutembelea wanafunzi chuoni hapo walikuwa wanajificha lakini wapi lazima askari na mashushushu watakukamata,” amesema mama huyo.

0 comments: