Na Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya imesema itachukua hatua za kisheria kwa wananchi
wanaovamia na kuchimba mchanga katika eneo la makaburi ya Mwanakwerekwe.
Hayo
yameelezwa leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ
Haji Omar Kheri alipokuwa akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la
Magomeni aliyetaka kujua hatua zinazotumika kwa wale wanaoendelea
kuchimba mchanga katika eneo la makaburi Mwanakwerekwe.
Amesema
sio vizuri wananchi kuendelea kuchimba mchanga katika eneo hilo la
makaburi kwani kufanya hivyo ni kitendo cha kikatili na hatua kali za
kisheria zitachukiwa kwa yeyote atakaekamatwa anafanya hivyo.
“Nawasihi
sana wananchi katika kufanya vitendo hivi kuwa jambo hili sio zuri
watafakari, kuwafanyia hivyo marehemu ni tendo ovu haistahiki ni kitendo
cha kinyama dini zote zinakataza kufanya hivyo”, alieleza.
Aidha
amesema Serikali inafahamu kuwa wananchi wanachimba mchanga katika eneo
hilo hivyo itafanya juhudi kubwa za kuwadhibiti wale wote wataokamatwa
na vitendo hivyo.
Waziri
Kheir amefafanua kuwa Wizara yake inaendelea kuwashajihisha wananchi
pamoja na kuandaa utaratibu wa kutoa michango ili kuweza kuhifadhi eneo
hilo lisiendelee kuvamiwa
Hata
hivyo alisema Serikali imepanga kulitumia eneo la Kama, lililozikiwa
watu waliofariki katika ajali ya MV. SPICE ISLANDERS, kuwa ni sehemu
mpya ya kuzikia waislamu ili kuondosha usumbufu.
Aidha
amefahamisha kuwa eneo la makaburi la Mwanakwerekwe limekuwa dogo
kutokana na kubadilika kwa matumizi ya ardhi ambapo eneo hilo lilikuwa
na ukubwa wa hekta 80 za mraba na zimebaki hekta 25 kutokana na
matumizi mengine ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment