HOME »
» MUME AMNYONGA MKE NA KUTUTUMBUKIZA CHOO CHA KANISA
|
Watu
watatu wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio matatu tofauti likiwemo la John
Kaguo (30) mkazi wa Usokami kumuua mkewe bi Jane Makombe (25) mkazi wa Lutuna
kwa kumnyonga shingoni na kisha kumtumbukiza kwenye choo cha kanisa.
Mwandishi wa mtandao huu Diana Bisangao kutoka Iringa anaripoti kuwa , Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 25 januari usiku huko maeneo ya
kijiji cha Ihalimba kata ya Ihalimba tarafa ya Kibengu wilaya ya Mufindi.
Mungi
alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano Zaidi huku chanzo cha tukio
hilo la kinyama likichunguzwa.
Na
katika tukio lingine bi Neema Luwumba (33) mkazi wa Lugalo alifariki dunia
katika Hospitali ya mkoa alipokuwa akiendelea na matibabu baada ya kupigwa na
shoti ya umeme maeneo ya Mkimbizi.
Kamanda
Mungi alisema marehemu alikutwa na janga hilo la kupigwa na shoti alipokuwa
akianika nguo alizokwisha kuzifua katika kamba inayosadikika kuwa ni waya wa
umeme.
Mbali
na matukio hayo mawili, Kamanda Mungi alisema mwanaume mmoja jina Juma Cheles
(60) alifariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na pikipiki huko maeneo ya kijiji cha Nzivu Mafinga
wilaya ya Mufindi.
Marehemu
alikuwa akiendesha pikipiki aina ya sunlg yenye namba za usajili T 609 BHJ
aligongana na pikipiki yenye namba za usajili T 268 BZR Sunlg mali ya Benedict
Mwanjombe (30) na kufariki papo hapo, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa ni
mwendo kasi.
|
0 comments:
Post a Comment