Thursday, 26 December 2013

MAN CITY YAIPIGA LIVERPOOL, 2-1 ANGALIA MATOKEO YAMECHI ZOTE ZA LEO

KOMPANY

Manchester City wameishusha Liverpool, ambao kabla ya Mechi za leo walikuwa kileleni, hadi Nafasi ya 4 na wao kupanda hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Arsenal baada kuichapa Liverpool Bao 2-1 Uwanjani Eithad.
Bao zote katika Mechi hii zilifungwa Kipindi cha Kwanza kwa Liverpool kuongoza kwa Bao la Philippe Coutinho na Vincent Kompany kusawazisha lakini kabla tu ya Mapumziko Alvaro Negredo alimzidi maarifa Kipa wa Liverpool Simon Mignolet na kupachika Bao la ushindi.

MAGOLI:
Man City 2
-Kompany Dakika ya 31
-Negredo 45
Liverpool 1
-Coutinho Dakika ya 24
 Refa wa mchezo : Lee Mason
Msululu wa Mechi hizi za Ligi Kuu England utaendelea Jumamosi na Jumapili lakini Bigi Mechi ni ile ya Jumapili huko Stamford Bridge wakati Chelsea itakapocheza na Liverpool.



CHELSEA YAPATA POITI 3 KWA GOLI MOJA TU!BPL2013LOGO
NEWCASTLE YAFUMUA 5!

RATIBA/MATOKEO:
Alhamisi Desemba 26
Hull City 2 Man United 3
Aston Villa 0 Crystal Palace 1
Cardiff 0 Southampton 3
Chelsea 1 Swansea 0
Everton 0 Sunderland 1
Newcastle 5 Stoke 1
Norwich 1 Fulham 2
Tottenham 1 West Brom 1
West Ham 1 Arsenal 3
  Man City 2 v Liverpool 1

CHELSEA 1 SWANSEA CITY 0
Bao la Dakika ya 29 la Eden Hazard limewapa Chelsea ushindi wa Bao 1-0 Nyumbani kwao Stamford Bridge walipocheza na Swansea City.
Chelsea sasa wamepanda hadi Nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya man city na Arsenal 

Refa: Mike Jones

EVERTON 0 SUNDERLAND 1
Penati ya Dakika ya 25 ya Ki Sung-Yeung, ambayo ilisababisha Kipa Tim Howard wa Everton apewe Kadi Nyekundu kwa kumwangusha Ki Sung-Yeung, imewapa ushindi mkubwa Sunderland wakiwa Ugenini Goodison Park.
Huu ni ushindi wa kwanza wa Sunderland wa Ugenini toka Mwezi Aprili lakini bado wapo mkiani.

Refa: Lee Probert

NORWICH CITY 1 FULHAM 2
Bao la Dakika ya 87 la Kiungo Scott Parker limewapa Fulham ushindi wa Bao 2-1 walipocheza Ugenini na Norwich City.
Gary Hooper ndie aliewapa Norwich Bao la kuongoza na Pajitim Kasami kusawazisha.

Refa: Jonathan Moss

NEWCASTLE 5 STOKE CITY 1
Newcastle walitoka nyuma kwa Bao la Oussama Assaidi na kuinyuka Stoke Bao 5 kwa Bao za Loic Remy, Bao 2, Goffran, Cabaye na Papiss Cisse, kwa Penati.

Refa: Martin Atkinson

WEST HAM 1 ARSENAL 3
Arsenal, wakicheza Ugenini huko Upton Park, walitoka nyuma kwa Bao la Carlton Cole na kupiga Bao 3 kupitia Theo Walcott, Bao 2, na Lukas Podolski.
Ushindi huu umewarudisha Arsenal kileleni  baada man city  kuwachapa Liverpool  2-1   huko Etihad.

Refa: Phil Dowd

TOTTENHAM 1 WEST BROM 1
Tottenham walibanwa mbavu na West Brom katika Mechi waliyocheza White Hart Lane na kutoka Sare 1-1.
Bao zilifungwa na Christian Eriksen, Dakika ya 36, na Jonas Olsson, Dakika ya 38.

Refa: Anthony Taylor
CARDIFF CITY 0 SOUTHAMPTON 3
Bao za Jay Rodriguez na Rickie Lambert leo zimewapa ushindi wa Ugenini Southampton wa Bao 3-0 walipocheza na Cardiff City.

Refa: Andre Marriner
ASTON VILLA 0 CRYSTAL PALACE 1
Bao safi sana la Dwight Gayle la Dakika ya 90 limewapa Crystal Palace ushindi wa Bao wa Ugenini walipocheza na Aston Villa na kuwang’oa kutoka Timu 3 za mkiani.
Gayle alianzia Benchi na kuingizwa Dakika ya 72.
Hiki kipigo cha 4 mfululizo kwa Aston Villa.

Refa: Howard Webb

MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 18 18 39
2 Man City 18 32 38
3 Chelsea 18 15 37
4 Liverpool 18 22 36
5 Everton 18 12 34
6 Newcastle 18 6 33
7 Man Utd 18 9 31
8 Tottenham 18 -5 31
9 Southampton 18 7 27
10 Stoke 18 -8 21
11 Swansea 18 -1 20
12 Hull 18 -7 20
13 Aston Villa 18 -7 19
14 Norwich 18 -15 19
15 West Brom 18 -5 17
16 Cardiff 18 -15 17
17 Crystal Palace 18 -15 16
18 Fulham 18 -16 16
19 West Ham 18 -10 14
20 Sunderland 18 -17 13

RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 28
1545 West Ham v West Brom
1800 Aston Villa v Swansea
1800 Hull v Fulham
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Norwich v Man United
2030 Cardiff v Sunderland
Jumapili Desemba 29
1630 Everton v Southampton
1630 Newcastle v Arsenal
1900 Chelsea v Liverpool
1900 Tottenham v Stoke
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham

0 comments: