Friday, 27 December 2013

HABARI NI KUWA FOLENI KUENDELEA KUTESA D'SALAAM MUDA HUU

 
Foleni jijini Dar es salaam

Kuna kila dalili kuwa jinamizi la foleni litaendelea kuwatesa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa muda mrefu zaidi kutokana na kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara za pembezoni (ring roads) na usanifu wa barabara za juu (flyig overs) ambayo kwa ujumla inahitaji walau Sh. bilioni 170.

Kero hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa ikiwa fedha hizo zitapatikana ili kutekeleza miradi mbalimbali iliyopewa kipaumbele katika kukabili tatizo hilo.


Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE hadi kufikia mwisho wa wiki iliyopita, umebaini kuwa ujenzi wa barabara za pembezoni unaendelea kwa kasi ya kinyonga huku ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara kuu ukiwa ndiyo kwanza uko katika hatua ya usanifu.


Aidha, jumla ya Sh. bilioni 171.2, ambazo ni sawa na asilimia 14 ya bajeti yote ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka huu wa fedha wa 2013/2014, ni sehemu tu ya mikakati iliyopewa kipaumbele katika utekelezaji ili kupunguza foleni jijini Dar es Salaam ikihusisha usanifu wa barabara za juu (Sh. bilioni 100), ujenzi barabara ya Kigogo – Jangwani (Sh. bilioni 7.6), fidia kwa majengo ya kandoni mwa barabara ya Kigogo-Jangwani (Sh. bilioni 15.8) na kipande cha kilomita tatu cha barabara ya Kimara Korogwe- Kilungule

27th December 2013

0 comments: