Friday, 27 December 2013

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NI NYENZO YA MAENDELEO

ti la leo

Banner

Ijumaa, Desemba 27, 2013 05:49 NA IBRAHIM HARUNA LIPUMBA
SEPTEMBA 27, mwaka huu serikali ililifungia gazeti la Mtanzania kwa madai kuwa limekuwa likiandika habari za kichochezi. Habari zilizodaiwa ni za kichochezi ni makala yenye kichwa cha habari kisemacho ‘URAIS WA DAMU” iliyochapishwa Machi 20, 2013, Makala ya uchambuzi yenye kichwa cha habari kisemacho “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI” iliyochapishwa  Juni 12, 2013. Habari ya tatu ni ile iliyochapishwa  Septemba 18, 2013 yenye kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU”.

Makala ambayo nakumbuka kuwa niliisoma vizuri ni ya Urais wa Damu. Hoja ya msingi ya makala hiyo ni kuwa “makundi yanayohasimiana ndani ya vyama vikuu vya siasa kwa sababu ya kusaka ukuu wa dola mwaka 2015, yako tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha yanafanikisha malengo ya kuupata urais baada ya rais wa sasa, Jakaya Kikwete, kumaliza muda wake.” Binafsi uchambuzi wa makala hii niliupenda pamoja na kuwa sikukubaliana na hoja zote. Mimi ni mzalendo kidankidanki. Nilipoisoma makala hii sikufikiria hata kidogo kuwa ni ya kichochezi. Hisia za makundi ndani ya vyama vya siasa kutumia vyombo vya dola kuhujumiana vinasababishwa na serikali kushindwa kuwakamata waliohusika na vitendo vya kuwatesa watu kama vile Dk. Ulimboka Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari na Absalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  New Habari (2006) Ltd.


Bila kujali kama makala haya ni ya kweli au la, Sheria ya Magazeti namba 3 ya mwaka 1976 iliyotungwa wakati wa ukiritimba wa chama kimoja na iliyotumiwa kulifungia gazeti la Mtanzania kwa muda wa miezi mitatu ni ya kikandamizaji, inayobana uhuru wa vyombo vya habari na kuiminyima demokrasia.

Sheria hii inaipa mamlaka serikali kuwa mlalamikaji, muendesha mashtaka na jaji wa kutoa hukumu. Haki haiwezi kutendeka katika hali hii.

Sheria hii inapinga kifungu cha 19 cha Taarifa ya Ulimwengu kuhusu haki za Binadamua kinachoeleza “Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa kushikilia maoni yake bila kuingiliwa kati, na uhuru wa kutafuta na kutoa habari na maoni kwa njia yoyote bila kujali mipaka.”

Katika nchi inayojenga au yenye mfumo wa demokrasia ya kweli, vyombo vya habari vinahesabiwa kama muhimili wa nne baada ya serikali, bunge na mahakama.

0 comments: