ASHANTI, JKT RUVU KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI JAN 1
MAOMBI YA TIKETI HUPITIA MPESA, FAHARI HUDUMA & CRDB SIMBANKING!!
SOMA ZAIDI:
Release No. 215
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 26, 2013
ASHANTI, JKT RUVU KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI JAN 1
Timu za Ligi Kuu za Ashanti United na
JKT Ruvu Stars zinapambana Januari Mosi mwakani kati moja ya mechi za
kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamzi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza
saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana
kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea
kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika.
Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza
tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye
Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega,
Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment
Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.
Ghomme Health & Education
Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance
Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB
Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly
Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.
Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa
Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers
Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors
Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa
Boko.
Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa
njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata
namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya
malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi
(business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao
anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.
Baada ya kufanya maombi kupitia njia
yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki
atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine
maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye
maeneo yafuatayo;
Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la
Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la
Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya
CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment