Dodoma
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na NIPASHE, wakazi hao walisema kuwa ofisa huyo kwa kutumia cheo chake, amegeuza jengo la ofisi kama mahakama ya kuwahukumu wananchi bila kufuata kanuni na taratibu za kisheria.
Walisema kuwa Manji anatumia madaraka yake vibaya kwani ofisi yake imekuwa ikitumika kutoa hukumu kwa vifungu vya kisheria visivyo rasmi. Mbali na hilo, pia wakazi hao walimtuhumu kuchochea migogoro ya ardhi miongoni mwao na kusababisha ukosefu wa amani.
Aidha, waliongeza kuwa Afisa Mtendaji huyo tangu awasili katika kituo hicho mwaka 2011, hajawahi kuitisha mkutano mkuu wa wananchi kwa ajili ya kuwasomea mapato na matumizi.
Walisema kutokana na shutuma hizo, wananchi hao hawana imani naye na wamemuomba Mkurugenzi kumuondoa ili kuwapo na amani.
Akijibu tuhuma hizo, Manji alisema kuwa tuhuma hizo ni propaganda za kisiasa ambazo zinazofanywa na kikundi kidogo cha wahuni wasiopenda maendeleo ndani ya jamii wa mtaa huo.
“Siyo kweli mimi natumia jengo langu kama mahakama wakati sheria na taratibu zinafahamika. Hao ni wakazi ambao hawataki kutii serikali iliyopo na ndiyo maana wanapohukumiwa kwa kutozwa faini kwa mujibu wa sheria ndogo za Manispaa, wanaona kama wamehukumiwa kinyume,” alisema Manji. Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Mtumba, William Njelimuyi, alikiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wake na kudai kuwa mtendaji hana ushirikiano na wenzake.
“Huyu Mtendaji wangu kwa kweli wananchi wangu wa mtaa huo wanamshutumu mambo mengi sana na kila nikimuuliza kuhusu utendaji wake huo anadai yeye anafanya kazi na Mkurugenzi tu hawezi kufanya na viongozi wasiomtakia mafanikio yake ya kiutendaji,” alisema diwani huyo.
Njelimuyi alisema kuwa kutokana na vitendo vyake hivyo, wakazi wa mtaa huo walishapeleka malalamiko yao kwa Mkurugenzi ili aondolewe, lakini mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kumwajibisha.
SOURCE:
NIPASHE
27th December 2013
0 comments:
Post a Comment