katibu wa kikao cha uteuzi wa
wanafunzi Bi Wamoja Ayub ambae ni katibu tawala mkoa akifunga kikao
cha uteuzi ,kulia kwake ni ofisa elimu msingi mkoa Bw Joseph
Mwinyikambi
...........................................................................................................................
SERIKALI
mkoani Iringa imepongeza ufaulu mzuri wa wanafunzi wa darasa
la saba mwaka huu 2013 kuwa ni ufaulu mzuri uliouwezesha mkoa
wa Iringa kushika nafasi ya tatu kitaifa kati ya mikoa 25 Tanzania
bara ,huku ukimlilia mwanafunzi mmoja wa shule ya Msingi Mabaoni
wilayani Mufindi ambae amefutiwa matokeo yake kutokana na
udanganyifu .
Huku
wabunge wawili kati ya 9 waliohudhurika kikao hicho akiwemo
Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigola na mbunge wa
jimbo la Mufindi Kaskazin Bw Mahamudu Mgimwa wakiipongeza wizara ya
elimu na mafunzo ya ufundi kutokana na utendaji kazi mzuri kwa
kuwezesha watahiniwa wanafunzi 14,956 wakiwemo wavulana 7,042
na wasichana 7,914
sawa na asilimia 65.25 mkoani Iringa kuchaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza
mwaka 2014.
Akizungumza leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati wa kikao cha
uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba
mwaka huu , katibu wa kikao hicho Wamoja Ayub ambae ni katibu
tawala wa mkoa wa Iringa alisema kuwa mkoa wa Iringa unajivunia
kuendelea kushika nafasi ya tatu kwa miaka miwili mfululizo sasa.
Hata
hivyo alisema kuwa lengo la mkoa wa Iringa kwa mwakani kuongeza
jitihada zaidi ili ikiwezekana kuushusha mkoa wa Dar es Salaam
katika nafasi ya Kwanza na Kilimanjaro katika nafasi ya pili na mkoa
wa Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa
la saba mwakani 2014
Kuhusu
udanganyifu katika mitihani alisema kuwa suala hilo lina madhara
makubwa kitaifa na kuwa suala hilo limekuwa likipigiwa kelele na
serikali kutokana na athari zake kuwa kubwa kwa wanafunzi
wanaohusika na udanganyifu kama ilivyo kwa mwanafunzi Atupelye Mligo
wa shule ya Msingi Mabaoni Mufindi aliyefutiwa matokeo yake .
Pia
alisema kwa mwalimu aliyehusika na tukio hilo la udanganyifu
mwalimu Edwin Ambokele wa shule ya msingi Makungu kwa sasa kesi
yake ipo mahakamani akisubiri mkono wa sheria unasemaje katika
suala hilo.
Bi
Wamoja alisema kuwa jambo hilo ni la aibu kwa mkoa wa Iringa na
Taifa kwa ujumla hivyo
aliwaonya walimu na maofisa elimu mkoani Iringa kuendelea kukemea
suala hilo ili lisije tokea tena katika mkoa wa Iringa .
Aidha
aliwataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya kusimamia ujenzi wa
vyumba vya madarasa ili kuwezesha wanafunzi waliochaguliwa kuanza
masomo kwa wakati hasa akisisitiza zaidi kwa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi
waliochaguliwa kuliko idadi ya vyumba vya madarasa kuhakikisha
wanakamilisha mapema ujenzi wa shule ya sekondari Nduli ili
wanafunzi waliopangwa katika shule hiyo kuanza masomo kwa wakati.
Akisisitiza
juu ya malengo ya matokeo makubwa sasa katika sekta ya elimu
alisema kuwa Manispaa ya Iringa inapaswa kufikia asilimia 90 kwa
mwaka 2014 wakati Halmashauri ya Iringa ina lengo la
kufikia asilimia 76 wakati Kilolo ni asilimia 77 huku Hlamshauri
ya Mufindi inalengo la kufikia asilimia 79 kuwa hayo ni malengo
yaliyopo katika utekelezaji wa matokeo makubwa sasa katika mkoa
Hata
hivyo baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wameeleza kusikitishwa
kwao na hatua ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi
kushindwa kushiriki katika kikao hicho nyeti na kuwaacha
wabunge wawili pekee wa jimbo la Mufindi kusini na Kaskazini
kushiriki kikao hicho huku wengine wote wakishindwa kutokea .
Wabunge wanaounda mkoa wa Iringa ni
Prof Peter Msolla Kilolo( CCM) mchungaji Peter Msigwa -Chadema Iringa
mjini, Dr Wiliam Mgimwa - Kalenga (CCM)Mahamundu Mgimwa - Mufindi
kaskazin ( CCM)Mendrady Kigola - Mufindi kusini (CCM) Wiliam Lukuvi -
Isimani (CCM ) ,Ritta kabati - Viti maalum (CCM)-Lediana Mafulu - Viti
maalum (CCM) na Chiku Abwao -Viti Maalum (Chadema)
Mbunge wa Kalenga Dr Mgimwa yawezekana ameshindwa kufika kutokana na sababu ya kiafya inayomsumbua na yupo nje ya nchi wakati mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi pia yawezekana ameshindwa kufika kutokana na majukumu ya nafasi yake ya uwaziri.
Mbunge wa Kalenga Dr Mgimwa yawezekana ameshindwa kufika kutokana na sababu ya kiafya inayomsumbua na yupo nje ya nchi wakati mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi pia yawezekana ameshindwa kufika kutokana na majukumu ya nafasi yake ya uwaziri.
Akitangaza
matokeo hayo kwa mkoa wa Iringa afisa elimu msingi Bw Joseph
Mwinyikambi alisema kuwa jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani
huo mwaka huu ni 14956 sawa na asilimia 65.2 na waliofaulu ni
14,956 sawa na asilimia 65.2 huku wanafunzi 7966 wakiwemo wasichana
4378 na wavulana 3588 sawa na asilimia 34.8 wakifeli katika mtihani huo
Huku
wanafunzi 226 wakishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu
mbali mbali idadi yake kwenye mabano ,utoro (196),vifo (12), ugonjwa
(13) na mimba (5).
Wakati
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yenye idadi ya shule za msingi 47
ikiongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo sasa
ikifuatiwa na Halmashauri ya Iringa yenye shule 138 kwa kushika
nafasi ya pili wakati Kilolo yenye shule 101 ikishika nafasi ya tatu
na Mufindi yenye shule 163 ikishika nafasi ya mwisho katika matokeo
hayo.
0 comments:
Post a Comment