Friday, 27 December 2013

WABUNGE WASIWE CHANZO CHA AMANI YETU KUTOWEKA

 
Donatus Kingazi

Paroko wa Kanisa la Katoliki kigango cha Mlingano wilayani Muheza, Donatus Kingazi, amesema nchi ya Tanzania ni kisiwa cha amani lakini hivi sasa amani hiyo inatoweka kutokana na migogoro ya kisiasa ndani ya Bunge na kutaka wabunge kukemewa pepo ndani ya bunge ili amani irejee.

Kingazi aliyasema hayo juzi katika ibada ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika kigango cha Mkanyageni Mnarani na kuhudhuriwa na mamia ya waumini.


Alisema wanasiasa wamekuwa wakigombana Bungeni mjini Dodoma kitu ambacho kinapoteza amani ya nchi aliyoiacha Baba wa Taifa Kambarage Nyerere na kwamba wabunge wamekwenda pale kutetea wananchi na siyo kugombana.


Kingazi alisema kuwa kitendo cha wabunge kugombana wakiwa bungeni ni aibu na kutaka wakemewe kama kuna mapepo huko bungeni ili amani isipotee.


Alisema kwa sasa amani imepotea kila sehemu panavita kali ya wenyewe kwa wenyewe na hivyo watu kukimbia nchi zao huku watoto, wazee, wakina mama na vijana wanapata shida wengine wanauawa.


Kingazi alisema zipo dalili za amani kutoweka kwa kuwa na mfululizio wa matukio sasa vikongwe wanauawa ovyo, makanisa yanachomwa moto, kumwagiwa tindi kali viongozi wa dini pamoja na upendo kutoweka katika familia.


Aidha, alipiga marufuku mavazi yasiyo ya heshima ambayo ni kinyume na maadili na kwamba kwa sasa baadhi ya wanawake wanavaa nguo fupi na wanaume kuvaa mlegezo ambayo hairidhishi. 
SOURCE: NIPASHE
27th December 2013

0 comments: