Sunday, 29 December 2013

CCM: WANAOTETEA SERIKALI TATU MAMLUKI

 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuia

Wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajia kukabidhi rasimu ya pili ya Katiba Mpya leo, Chama Cha Mapinduzi kimesema mfumo wa serikali tatu unaotetewa na wapinzani nchini ni hatarishi na unaweza kuvunja Muungano.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuia, wakati akifungua mkutano maalum wa CCM wa Mkoa wa Magharibi uliotathmini utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na hali ya kisiasa katika kipindi cha miaka 50 ya Mapinduzi.


Aidha, alisema mfumo wa Muungano wa serikali mbili umesaidia kujenga Muungano imara kwa miaka 50 na kuwataka wananchi wasikubali kampeni ianyofanywa ya kutetea mfumo wa serikali tatu na kusema mfumo huo si imara na salama kwa amani na utulivu wa Taifa. 
 
SOURCE: NIPASHE
30th December 2013

0 comments: