Wednesday, 25 December 2013

BAADHI YA VITUO VYA TV VYASITISHA MATANGAZO YAO KENYA

 Rais Uhuru Kenyatta akipunga mkono wakati wa sherehe ya siku ya Mashujaa.
Baadhi ya vituo vikuu vya televisheni nchini Kenya vilisitisha matangazo yao Jumatatu usiku baada ya mahakama kuu kutpilia mbali maombi yao ya kutaka muda zaidi wa kubadilisha vyombo vya mfumo wa analog kuelekea mfumo wa digital.
Mashirika makuu ya Nation Media, Standard na Royal media service yaliwasilisha maombi mbele ya mahakama kuu mwezi liyopita kutaka kupewa muda zaidi kabla ya kubadilisha mfumo wa digitali ambao ulibidi kuanza Disemba 23, 2013 huko Kenya.
Kutokana na hatua hiyo mamilioni ya watazamaji na mashabiki wa vituo vya NTV, KTN citizen QTV na vituo vingine hawakuweza kuona matangazo yao na vipindi wanavyopenda.(P.T)
Baada ya kushindwa mawakili wa vituo hivyo vitatu walisema hawana budi bali kuheshimu sheria lakini wamesema wanafikisha malalamiko yao mbele ya mahakama ya ruifaa Jumanne katika lengo la kubadili uwamuzi wa jaji Majanja.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Mawasiliano Kenya CCK, Francis Wangusi anasema hatua walochukua wamiliki wa vituo hivyo vya televisheni, kufunga matangazo yao bila ya kushauriana na tume yake inakwenda kinyume na sheria . Na watajaribu kujadiliana nao kufahamu kinachotendeka.
Jaji huyo alikataa pia pendekezo la mashirika hayo ya televisheni kupewa muda wa siku 30 kuzima matangazo yao ya analogue na kubadilisha katika digitali.

Kufuatana na tume ya mawasiliano ya kenya CCK utaratibu ulibidi kuanza tarehe 13 disemba lakini mahakama ilichelewesha kwa siku 10 ili kusubiri uwamuzi wa jaji hiyo Jumatatu.

CHANZO BBCSWAHILI.COM

0 comments: